Wawakilishi wa kisiasa wa Kenya jana waliwachagua maspika wa baraza la seneti na bunge la jipya la nchi hiyo. Wanachama wa muungano wa Jublee, Bw Muturi amechaguliwa kuwa spika wa bunge, na mbunge wa zamani Bw Ekwee Ethuro amechaguliwa kuwa spika wa seneti.
Bw Muturi alimshinda mgombea wa muungano wa CORD Bw Keneth Marende kwa kura 219 dhidi ya 129. Na Bw Ethuro alimshinda Maalim Farah kwa kupata kura 38 dhidi ya 29.
Muungano wa Jubilee una viti vingi kwenye bunge la Kenya, na sheria mpya ya Kenya inataka mtu kushinda uchaguzi kwa kupata theluthi mbili ya kura zitakazopigwa.
Baada ya kupata ushindi Bw Muturi alilihutubia bunge na kumpongeza mtangulizi wake kwa kuongoza mchakato wa utungaji wa sheria katika bunge lililopita. Bw Ethuro aliahidi kuwa atasimamia utawala wa sheria
No comments:
Post a Comment