Rais wa China Xi Jinping kushoto akiwa na Jackob Zhuma wa A. Kusini |
Akizungumza na rais Zuma jana huko Pretoria, rais Xi amesema China inaunga mkono juhudi za Afrika Kusini za kusaidia nchi za Afrika kujipatia maendeleo kwa pamoja na kujiamulia mambo yao.
Amesema China inapenda kushirikiana na Afrika Kusini katika
mambo ya waafrika, kuunga mkono ushirikiano kati ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika na "Mpango wa Ushirikiano Mpya Maendeleo ya uchumi barani Afrika", kuhimiza ujenzi wa miundo mbinu na utandawazi wa uchumi barani Afrika, kushiriki kiujenzi kwenye mambo ya amani na usalama barani Afrika, ili kutoa mchango kwa ajili ya amani na maendeleo ya kudumu barani Afrika. Rais Zuma amesema China ni mshirika wa kwanza kibiashara wa Afrika Kusini, na nchi yake inatarajia makampuni mengi zaidi ya China yatawekeza nchini humo, kuendeleza mradi wa ushirikiano katika ujenzi wa miundo mbinu ili kuifanya biashara ya pande mbili iongezeke kwa uwiano.
Marais hao wawili pia walihudhuria hafla ya kusainiwa kwa nyaraka za miradi ya biashara, uwekezaji wa kifedha, madini, utamaduni na elimu pamoja na ujenzi wa miundo mbinu.
No comments:
Post a Comment