Na Prince
Akbar
KUANZIA saa 4:00 asubuhi ya leo, zoezi la usaili kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa klabu ya Yanga, uliopangwa kufanyika Julai 15, mwaka huu watakuwa wakifanyiwa usaili makao makuu ya klabu, makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani.
KUANZIA saa 4:00 asubuhi ya leo, zoezi la usaili kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa klabu ya Yanga, uliopangwa kufanyika Julai 15, mwaka huu watakuwa wakifanyiwa usaili makao makuu ya klabu, makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani.
Louis Sendeu, Ofisa Habari wa
Yanga, ameiambia BIN ZUBEIRY asubuhi hii kwamba zoezi hilo
litaongozwa na Kamati ya Uchaguzi, chini ya Mwenyekiti wake, Jaji John Mkwawa na
wagombea wote wanatakiwa kufika wao wenyewe.
Tayari Kamati hiyo ya Mkwawa,
imemuengua mgombea Nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Ally Mayay Tembele, kwa sababu
hakufika kusikiliza pingamizi dhidi yake.
Kuenguliwa kwa Mayay,
kunafanya nafasi ya Makamu Mwenyekiti ibakiwe na watu watatu, ambao ni Ayoub
Nyenzi, Yono Kevela na Clement Sanga na wote watafanyiwa usaili
leo.
Nafasi ya Uenyekiti wagombea
ni Yussuf Mehboob Manj, John Jambele, Edgar Chibura na Sarah
Ramadhani.
Katika nafasi za Ujumbe ni
Lameck Nyambaya, Ramadhani Mzimba ‘Kampira’, Mohamed Mbaraka, Ramadhani Said,
Edgar Fongo, Beda Simba, Ahmad Gao, Mussa Katabaro, George Manyama, Aaron
Nyanda, Abdallah Bin Kleb, Omary Ndula, Shaaban Katwila, Jumanne Mohamed
Mwammenywa, Abdallah Mbaraka, Peter Haule, Justin Baruti na Abdallah
Sharia.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya
Handeni, Muhingo Rweyemamu, Mfanyabiashara Muzamil Katunzi na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Madini, Eliakhim Masu walichukua fomu za kugombea Ujumbe lakini
wakashindwa kurudisha, wakati Isaac Chanzi pia hakurudisha fomu ya Makamu
Mwenyekiti hivyo moja kwa moja hao hawamo katika kinyang’anyiro.
Uchaguzi huo, unaokuja baada
ya Wajumbe wengi wa Kamati ya Utendaji katika uongozi uliokuwa madarakani,
akiwemo Mwenyekiti Wakili Lloyd Baharagu Nchunga na Makamu wake, Davis David
Mosha kujiuzulu utafanyika Julai 15, mwaka huu Dar es Salaam.
Tayari Kamati ya Uchaguzi ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilitoa onyo kwa wagombea ambao waliwasilisha
vyeti visivyostahili na kutaka wawasilishe vyeti vinavyotambulika kwa mujibu wa
taratibu za uchaguzi, ambavyo ni vyeti vya Baraza la Mitihani.
SILAHA ZA KISIWANI ZATINGA AZAM FC
Viungo Abdi Kassim 'Babbi' kushoto na Abdulhalim Humud 'Gaucho', baadhi ya wachezaji waliokuwa na timu ya taifa ya Zanzibar ambao tayari wameripoti Azam FC |
Na Prince
Akbar
WACHEZAJI wa Azam FC waliokuwa na timu ya taifa ya Zanzibar jana wamejiunga na wenzao kambini, kwa maandalizi ya klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, ingawa Waziri Salum aliripoti tu na kuondoka kutokana na matatizo.
WACHEZAJI wa Azam FC waliokuwa na timu ya taifa ya Zanzibar jana wamejiunga na wenzao kambini, kwa maandalizi ya klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, ingawa Waziri Salum aliripoti tu na kuondoka kutokana na matatizo.
Kutoka Azam, BIN
ZUBEIRY imeelezwa kwamba, Salum yeye mwenyewe ni mgonjwa na pili baba
yake anaumwa hivyo amerejea Zanzibar, lakini Abdi Kassim ‘Babbi’, Abdulhalim
Humud ‘Gaucho’, Abdulghani
Gullam na Hamisi Mcha wao
wameanza mazoeozi moja kwa moja na wenzao. Wachezaji wa Azam FC waliokuwa timu
ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wanatarajiwa kuanza mazoezi
Jumatatu.
Kiungo Salum Abubakar ‘Sure
Boy Jr.’ aliyeumia kabla ya Stars kwenda Msumbiji, yeye anaendelea na programu
maalum ya daktari wa timu hiyo na tayari ameripoti.
Azam FC inaendelea vema na
maandalizi yake ya Kombe la Kagame na leo asubuhi wanafanya mazoezi ya gym
kwenye Uwanja wa Chamazi.
Tayari Azam, washindi wa pili
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wamekwishamalisha usajili wa wachezaji wao
hata kabla ya kwenda likizo.
Programu ya maandalizi ya
Kombe la Kagame, inayoendelea hivi sasa itamalizika siku moja kabla ya kuanza
mashindano hayo, Juni 28 na yatakapomalizika, wachezaji watapewa mapumziko ya
siku chache kabla ya kuanza maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi
Kuu.
Maandalizi kwa ajili ya VPL
yatahusisha pia ziara ya nje ya nchi ya kujiandaa na msimu mpya, ingawa amesema
nchi hiyo itatajwa baadaye.
Wachezaji wapya kikosini Azam
msimu huu ni kiungo Mkenya George ‘Blackberry’ Odhiambo na kipa Deogratius
Munishi kutoka Mtibwa Sugar, wakati Aishi Salum, Jackson Wandwi, Dizana, Ibrahim
Rajab Jeba na Joseph Kimwaga, wamepandishwa kutoka akademi ya Azam.
Kikosi kamili cha Azam FC
kinaundwa; na makipa, Mwadini Ally, Deo Munishi ‘Dida’ Aishi Salum na Jackson
Wandwi, mabeki wa Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Samir Haji Nuhu,
Luckson Kakolaki, Said Mourad, Joseph Owino na Aggrey Morris.
Viongo ni Kipre Bolou,
Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum Abubakar, Abdi Kassim Sadalla, Ramadhani
Suleiman Chombo, Abdulghani Ghullam, Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz Stima,
Ibrahim Joel Mwaipopo, Kipre Tchetche, Mrisho Ngassa, Zahoro Pazi, Khamis Mcha
na George Odhiambo ‘Blackberry’ wakati washambuliaji ni Gaudence Mwaikimba, John
Bocco ‘Adebayor’.
Hii
ni mara ya kwanza kwa Azam FC kucheza Kombe la Kagame, baada ya kushika nafasi
ya pili katika msimu uliopita wa Ligi Kuu. Katika Kombe la Kagame mwaka huu,
wenyeji Bara wataingiza timu tatu, Yanga ambao ni mabingwa watetezi, wakati
Simba na Azam wanaingia kwa nafasi za uwakilishi.
MRWANDA ATUA NA 'EXCUSE' MAZOEZINI SIMBA, MILOVAN KUTUA DAR KESHOKUTWA
Na Prince
Akbar
WAKATI mshambuliaji Danny Mrwanda aliwasili kwenye mazoezi ya Simba SC jana Uwanja wa TCC Chang’ombe, Dar es Salaam, kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mserbia Milovan Cirkovick atatua Jumapili hii tayari kuanza kuiandaa timu kwa ajili ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, imeelezwa.
WAKATI mshambuliaji Danny Mrwanda aliwasili kwenye mazoezi ya Simba SC jana Uwanja wa TCC Chang’ombe, Dar es Salaam, kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mserbia Milovan Cirkovick atatua Jumapili hii tayari kuanza kuiandaa timu kwa ajili ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, imeelezwa.
Habari kutoka ndani ya Simba,
ambazo BIN ZUBEIRY zimesema kwamba Milovan atawasili Jumapili na
kukutana na uongozi ili kupanga programu rasmi ya maandalizi kwa ajili ya
michuano hiyo, ambayo Simba ni bingwa wake mara sita katika miaka ya 1975, 1991,
1992, 1995, 1996 na 2002.
Kwa
upande wake, Mrwanda aliyesajiliwa kutoka Dong Tam Long ya Vietnam, alifika
mazoezini jana jioni, lakini hakufanya na ameahidi kuanza rasmi timu
itakaporejea katika ziara yake ya Kanda ya Ziwa, ambako pamoja na kwenda
kutambulisha Kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu, wanakwenda kucheza mechi za
kirafiki. Simba imeondoka leo Dar es Salaam.
YANGA WAANZA MAZOEZI YA UFUKWENI
Nizar Khalfan, moja ya silaha mpya Yanga |
KLABU bingwa Afrika Mashariki
na Kati, Yanga kesho asubuhi inatarajiwa kuanza mazoezi ya ufukweni katika
ufukwe wa Coco Beach, Dar es Salaam ili kuwajengea stamina wachezaji
wake.
Ofisa Habari wa Yanga, Louis
Sendeu ameiambia BIN ZUBEIRY asubuhi hii kwamba baada ya programu
ya mazoezi ya ufukweni, wachezaji hao watapelekwa gym na baada ya hapo wataingia
kambini moja kwa moja wiki ijayo.
Yanga inajiandaa na michuano
ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame itakayofanyika Dar es
Salaam kuanzia Julai 14 hadi 29, mwaka huu ikishirikisha timu nyingine mbili za
Tanzania, bingwa wa Ligi Kuu, Simba SC na washindi wa pili, Azam FC.
Tayari wachezaji wapya
waliosajiliwa na Yanga wamekwishaanza mazoezi Uwanja wa Kaunda, akiwemo kipa wa
Simba, Ally Mustafa ‘Barthez’, Said Bahanuzi na Juma Abdul, wote kutoka Mtibwa
Sugar ya Morogoro na Nizar Khalfan aliyekuwa akichezea Philadelphia Union ya
Marekani.
Wachezaji wa zamani ambao hadi
sasa wamekwishafika Jangwani ni Juma Seif ‘Kijiko’, ambaye kulikuwa kuna tetesi
anakwenda Simba, Hamisi Kiiza, Kenneth Asamoah, Yaw Berko, Shamte Ally, Jerry
Tegete, Stefano Mwasyika, Godfrey Taita, Athumani Iddi ‘Chuji’, Oscar Joshua,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Idrisa Senga, Omega Seme na Ibrahim Job.
MODRIC NI KAMA AMEOTA MBAWA MAN UNITED
Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya
HULK ACHAGUA CHELSEA
MSHAMBULIAJIn wa Porto,
Hulk, mwenye umri wa miaka 25, ameiambia Paris St-Germain angependa zaidi
kujiunga na Chelsea, kwa dau la pauni Milioni 38 lililoripotiwa.
KLABU
ya Liverpool ina nia ya kumsajili mshambuliaji Fabio Borini, mwenye umri wa
miaka 21, ambaye amefunga mabao 10 katika mechi 26 alizoichezea Roma ya Italia,
hiivyo kuingia kikosi cha Italia cha Euro 2012. Kocha wa Wekundu hao, Brendan
Rodgers alipiga kazi na mpachika mabao huyo akiwa Chelsea na alimsajili kwa
mkopo The Blues baada ya kutua Swansea.
KLABU
ya Real Madrid inajiandaa kuilipa Tottenham pauni Milioni 30 kwa ajili ya
kumnasa Luka Modric, mwenye umri wa miaka 26, baada ya kocha Jose Mourinho
kuitaka klabu yake iongeze dau.
KLABU
ya Porto inaweza kujikuta inapoteza mchezaji mwingine, baada ya wakala wa
mchezaji wao anayetakiwa na Manchester United kumlenga James Rodriguez, mwenye
umri wa miaka 20, kusema mteja wake yupo katika mazingira magumu Porto.
OTHER GOSSIP
KOCHA
wa Manchester City, Roberto Mancini anaamini Italia wanatakiwa kumtumia Mario
Balotelli kama wanataka nafasi ya kuifunga England Jumapili.
KOCHA
wa Everton, David Moyes ameunga mkono wa kuchanga fedha kwa ajili ya ujenzi mpya
ambao watautumia kwa pamoja na wapinzani wao, Liverpool.
MUSTAKABALI
wa Joey Barton katika klabu ya Queens Park Rangers utaeleweka katika siku chache
zijazo, baada ya klabu hiyo kukamilisha uchunguzi wake wa ndani juu ya kadi
nyekundu aliyopewa katika mechi dhidi ya Manchester City ya kufunga msimuj
uliopita wa Ligi Kuu
No comments:
Post a Comment