SIMBA 2 TOTO AFRICAN 0
SIMBA leo imeichapa Toto
African ya Mwanza kwa mabao 2-0 katika pambano kali la kirafiki lililofanyika
katika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Hiyo ilikuwa ni mechi ya
kwanza ya kirafiki kwa Simba katika ziara yake ya mikoa ya kanda ya ziwa
iliyoanza jana (Juni 22) na kumalizika keshokutwa.
Wekundu wa Msimbazi walianza
pambano hilo kwa kasi na iliwachukua dakika 17 tu kuandika bao la kwanza
lililowekwa kimiani na Uhuru Selemani aliyemalizia vizuri pasi ya Abdallah
Juma.
Hadi kipindi cha kwanza
kinamalizika, Simba ilikuwa inaongoza kwa bao hilo moja.
Katika kipindi cha pili, Simba
ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Abdallah Seseme na Hassan Khatib na nafasi zao
kuchukuliwa na William Lucian (Gallas) na Jonas Mkude.
Mabadiliko hayo yalizaa
matunda kwani katika dakika ya 48, Simba iliandika bao la pili lililofungwa na
Salim Kinje, mchezaji mpya wa Simba aliyesajiliwa kutoka AFC Leopards ya
Kenya.
Kinje alifunga bao hilo
akiunganisha moja kwa moja kutoka nje ya 18 pasi ya kichwa kutoka kwa
Uhuru.
Katika pambano la jana,
wachezaji waliosajiliwa msimu huu walikuwa ni Waziri Hamad, Paulo Ngalema, Kiggi
Makassy, Kinje na Abdallah Juma.
Wachezaji wawili wa kikosi cha
vijana Simba maarufu kwa jina la U-20, Haruna Chanonga na Lucian pia walicheza
mechi yao ya kwanza kwa kikosi cha wakubwa leo hii.
Juni 24 Simba itaingia kwenye
uwanja wa Kambarage Shinyanga kupambana na mabingwa wa soka wa Uganda, Express
FC.
SIMBA; Waziri, Hassan
(Gallas), Ngalema (Omar Waziri), Obadia Mungusa, Haruna Shamte, Amri Kiemba
(Edward Christopher), Chanonga, Seseme (Kiggi), Abdallah (Ramadhani Salum),
Kinje na Uhuru.
MIYEYUSHO ALIVYOMTWANGA MMALAWI...
Bondia Francis Miyeyusho akimshambulia bondia kutoka
Malawi John Masamba wakati wa mpambano
wao uliofanyika Dar es salaam jana Miyayusho alishinda kwa K.O Raundi ya 5.picha
na www,superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia John Masamba kutoka Malawi akioneshana ufundi wa
kutupa masumbwi na Francis Miyeyusho
wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana. Picha na www.superdboxingcoach,blogspot.com
Bondia John Masamba kutoka Malawi akioneshana ufundi wa
kutupa masumbwi na Francis Miyeyusho
wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana. Picha na www.superdboxingcoach,blogspot.com
Bondia Obote ameme
akioneshana kazi na Cosimasi Cheka
Bondia Miyayusho
akisikiliza wimbo wa taifa wakati wa kuimba nyimbo za matasifa
mawili
Bondia Rashidi Ali
akioneshana kazi na Amnos Mwamakula wakati wa mpambano wao
jana
WEMA, DIAMOND 'BADO WAPENZI'
JANA katika ukumbi wa
Makumbusho, katikati ya Jiji la Dar es Salaam, mkabala na Chuo cha Usimamizi wa
Fedha (IFM), kulikuwa kuna onyesho la Miss Dar Inter College.
BIN ZUBEIRY
alikuwepo na kamera yake katika onyesho hilo, ambalo Jaji Mkuu alikuwa Miss
Tanzania wa 2006, Wema Sepetu huku mpenzi wake wa zamani, Nassib Abdul ‘Diamond
Platinum’ akitumbuiza.
Shoo ilichelewa kuanza kidogo
hadi mida ya saa sita usiku- na baada ya warembo kucheza shoo ya ufunguzi,
kupita na vazi la ubunifu na la jioni, kabla ya tano bora kutangazwa, ilikuwa
zamu ya Platinum wa bongo kupanda katika stage.
Taa zilizimwa na kijana
akaibuka na madansa wake jukwaani. Lakini wakati tu MC anasema anamuita Diamond,
mapigo ya moyo ya Jaji Mkuu, yalionekana kubadilika na kwenda kasi.
Kwa muda wote, Majaji wenzake
wawili walikuwa wanawasiliana naye, lakini ilionekana ghafla kama yeye amekata
mawasiliano nao.
Kulikuwa kuna dalili za
kutosha kusema; Wema alichanganyikiwa. Dida wa Times FC aliyekuwa jaji pia,
alijitahidi kadiri ya uwezo wake kumfanya Wema awe katika hali ya kawaida,
lakini alishindwa.
Wema alishindwa kujimudu.
Kulikuwa kuna dalili zsa kutosha kusema Wema anampenda sana Diamond. Alikuwa
anamfuatilia kwa kila hatua. Alikuwa anaingiwa na kuguswa na nyimbo za
Wema Wangu, Mawazo na Nimpende Nani alizokuwa
anaimba Diamond pale jukwaani.
Diamond naye sasa; ilionekana
dhahiri kila anachokifanya jukwaani ni kwa ajili ya Wema. Na alikuwa anaomba
sapoti ya mashabiki ili kujiridhisha kama yuko sahihi.
Kwa sisi waswahili huwezi
kusita kusema Diamond alikuwa anampiga ‘vikoleo’ aka vijembe Wema. Lakini pamoja
na yote, Diamond alionekana kuwasilisha hisia zake kwamba hakuwa tayari kuachana
na Wema.
Ni kama kuna kitu kilimsukuma
kujitoa katika mahusiano. Ni nini hicho? Kitendawili kigumu.
Ikumbukwe wawili hawa
walifikia hadi kuvalishana pete ya uchumba lakini ndani ya miezi michache tu,
penzi likavunjika.
Ila, ndani ya mioyo yao kuna
siri nzito sana na kinachoonekana anakosekana jasiri tu kati yao wa kumuanza
mwenzake kuhusu mada ya kurejesha uhusiano wao.
Wanaonekana wanapendana bado,
na haitakuwa ajabu siku moja wakirudiana. BIN ZUBEIRY mwenye
uzoefu wa kutosha juu ya masuala ya mahusiano, raha na maumivu ya mapenzi,
anawoambea wawili hao, siku moja wawe mwili mmoja tena. Mungu wabariki na
wafungue, waondolee uzito Wema na Diamond. Siku moja, waitane wife n husband.
Inshaallah. True love never die.
No comments:
Post a Comment