Wednesday, May 30, 2012

MEKUCHA UCHAGUZI YANGA SC
Katibu wa kamati ya uchaguzi ya Yanga Francis Kaswahili (pichani) akizungumzia uchaguzi huo ambapo amewataka wanachama wote ambao hawajalipa ada kufanya hivyo ili kuweza kushiriki katika mkutano huo.
Alisema kupitia uchaguzi huo zitajazwa nafasi za Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanne ambapo wanachama wayakaowania uongozi wanatakiwa kuwasilisha fomu zao wakiambatanisha risiti ya kununulia fomu, vyeti vya shule, uthibitisho wa uraia, namba ya uanachama na picha mbili za passport size.

STARS WAKABIDHIWA BENDERA, KUWAFUATA KINA DROGBA KESHO

NAibu waziri wa habari, vijana, Utamaduni na Michezo Amos makalla akimkabidhi bendera ya Taifa Nahodha wa Stars Juma Kaseja, wakati wa hafka ya kuiaga timu hiyo leo kwenye hoteli ya Tansoma.Stars inaondoka alfajir ya kesho kwenda Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wao wa mchujo wa komve la Dunia utakaopigwa juni mbil.Wengine ni meneja wa bia ya Kilimanjaro inayoidhamini9 timu hiyo George Kavise, Mwenyekiti wa BMT Dioniz Malinzi na Kocha wa Stars, Kim Poulsen.
Nahodha wa Stars Juma Kasejha akizungumza machache
Baadhi ya wachezaji wa Stars
Baadhi ya wachezaji waliohudhuria hafla hiyo leo

KOCHA STARS AWAASA NYOTA WAKE KUTOWAHOFIA KINA DROGBAA DROGBA


KOCHA mkuu wa timu ya Taifa Taifa Stars amewataka wachezaji wake kutohofia nyota waliopo katika kikosi cha Ivory Coast kwani hawana tofouti na wao.
Stars na Ivory Coast watkawaana Juni 2, mjini Abidjan, katika mechi ya kuwania kucheza fainali za kombe la
dunia ambapo kikosi cha Ivory Coast kinawachezaji wanaosakata soka la kulipwa barani Ulaya wakiwemo Didier Drogba, . Yaya Toure na Solomon Kalou na wengineo.
Kim alisema wanaiheshimu Ivory Coast kama moja ya timu yenye wachezaji wazuri lakini hawaihofii kwani wachezaji wa Stars pia ni wazuri ingawa wanatofaitiana vitu vidogo vidogo tu.
Kocha huyo aliwataka wachezaji wake kupambana kadiri wawezavyo katika mchezo huo kwani ndio siri ya ushindi na mafanikio ya timu yoyote.

NYOSO,UHURU SELEMAN WAITESA YANGA


KLABU ya Yanga imeanza mkakati wa kuwasajili wachezaji kadhaa kutoka kwa watani wao Simba, wakiwamo mabeki Juma Jabu, Juma Nyoso na kiungo Uhuru Suleiman.
Kwa mujibu wa habari zilizoifikia Tanzania Daima na kuthibitishwa na mmoja wa viongozi wa klabu hiyo anayehusika na usajili, wameamua kuwafukuzia nyota hao kutokana na mikataba yao Simba kukaribia mwishoni.
Chanzo hicho kimedokeza kuwa, kwa sasa wapo kwenye mazungumzo ya awali na nyota hao, ingawa bado hawajafikia hatua ya mwisho kwa ajili ya kusaini fomu za usajili kwa msimu ujao wa Ligi Kuu.

Yanga imekuwa na mkakati wa kusuka kikosi cha ushindi baada ya kushindwa kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu iliyofikia tamati Mei 6, ikimaliza nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam FC.
Kamaunavyojua, Yanga imekuwa mbovu katika siku za hivi karibuni na matokeo yake tulipoteza ubingwa wa Ligi Kuu Bara na nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa msimu ujao, sasa hatutaki kurudia makosa, tunataka kufanya usajili mzuri kurejesha heshima yetu,” alisema kiongozi huyo.
Aliongeza, mbali ya hao, pia wana mpango wa kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa kusajili wawili kutoka nchini Rwandaambao ni Meddie Kegere na Olivier Karekezi, waliong’ara kwenye michuano ya Kombe la Chalenji, lililofanyika Desemba, 2011, jijini Dar es Salaam.
Chini ya ufadhili wa Yusuf Manji aliyerejea kuokoa jahazi, Yanga wamepania kusajili nyota mahiri na kuajiri kocha bora atakayeziba nafasi ya Mserbia, Kostadin Papic, aliyemaliza mkataba wake mapema mwezi huu.

MISS DAR INTER COLLEGE YAZIDI KUSHIKA KASI

Baadhi ya warembo wanaowania taji la Miss Dar Inter College 2012 wakiwa katika pozi mara baada ya mazoezi yao ya kila siku yanayofanyika kwenye hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa warembo hao Marylydia Boniface akiwapa maneno mawili matatu warembo hao.

VIONGOZI WAPYA RT WAANZA MIKAKATI

BAADHI ya viongozi wapya wa chama cha Riadha Tanzania (RT) wakijadiliana masuala mbalimbali kuhusiana na chama hicho mara baada ya kuchaguliwa hivi karibuni.
Kutoka kushoto ni Tullo Chambo (Mjumbe) Suleiman Is-haq (Mweka Hazina) na Suleiman Nyambui (Katibu Mkuu) pamoja na mdau wa mamapipiro blog, Maria Kayala.


STAMINA TATIZO LA WACHEZAJI TANZANIA-POILSEN



WAKATI kikosi cha timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, kikitarajia kuondoka alfajiri ya kesho kwenda Ivory Coast kwa mechi ya kimataifa, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen, amesema stamina ni tatizo kubwa kwa nyota wengi.
Poulsen aliyetwaa jukumu hilo hivi karibuni kutoka kwa Jan Poulsen, aliyasema hayo jana wakati akitoa tathmini fupi juu ya mazingira ya kikosi chake tangu akabidhiwe jukumu hilo wiki mbili zilizopita.
Alisema, pamoja na wachezaji wengi kuwa na uwezo mkubwa kiuchezaji, suala la stamina limekuwa tatizo kwa wachezaji wengi, hivyo kushindwa kucheza kwa kasi na ufanisi kwa dakika zote 90.
Alisema kutokana na dosari hiyo, tayari ameanza kuchukua hatua kwa kufanya mazungumza na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuangalia njia bora ya kuondoa tatizo hilo kwa kushirikiana na makocha wa timu nyingine.
“Kwa upande wa Stars, nimeshaanza nalo kwa kuwapa mazoezi ya ziada baada ya mazoezi ya kawaida. Kwa kweli, wachezaji wameonekana kuyakubali, wameridhishwa nayo na kuyafurahia, binafsi inanitia moyo,” alisema.
Kim alisema mbali ya stamina, pia amekuwa akiwasihi wachezaji wake kuwa na moyo wa kujituma, akisema hicho ni kitu muhimu kwa timu katika kupigania ushindi na mafanikio ya timu.
Aidha, Poulsen alisema ndani ya kipindi cha wiki mbili alizodumu na timu hiyo, wachezaji wameanza kuelewa falsafa yake, hivyo kumpa matumaini ya kuwa na kikosi bora zaidi katika siku za usoni.
Hata hivyo, ameishauri TFF kuwa, wachezaji wote ambao watakuwepo kambini kipindi cha maandalizi ya mechi, wote wawe wanasafiri na timu (hata kama hawatacheza), kwa lengo la kuwapa nafasi ya kujifunza zaidi.
Katika hatua nyingine, Kim amekana kufanya upendeleo katika uteuzi wa kikosi cha kwanza, hasa katika mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi, akisema alichagua kutokana na uwezo na sifa zao.
Aliongeza kuwa, nyota wake Nurdin Bakari na Thomas Ulimwengu watabaki kutokana na kuwa majeruhi waliyopata wakati wa mazoezi yao, hivyo watabaki kujinoa kabla ya kuungana na wenzao watakaporudi kujiandaa dhidi ya Gambia.
Nyota wa Stars ni makipa: Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar). Mabeki: Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).
Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba - U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).
Washambuliaji ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano (Simba -U20), Simon Msuva (Moro United - U20), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam).

No comments: