Tuesday, July 15, 2014

UJERUMANI WAPOKELEWA KWA SHANGWE LA KUFA MTU, HUKU JEZI ZA 4 STARS ZIKISHINE

 



Timu ya taifa imewasili nchini humo kwa kishindo
 
Na Juma Mohamed
 
Timu ya taifa ya soka ya Ujerumani imewasili nchini humo kwa kishindo wakiwa na kombe lao la ushindi walilolinyakua katika mashindano ya kombe la dunia ambyo yalikamilika juzi nchini Brazil.
Maelfu ya mashabiki wa soka wamekuwa wakisubiri tangu asubuhi na mapema mjini Berlin kuwakaribisha wachezaji hao.
 
Sherehe zitafanyika katika eneo la Brandenburg Gate, ambako wachezaji wataonyeshea kombe lao, ambalo walilishinda katika fainali ya mashindano hayo dhidi ya Argentina.

 
Wengi wamepokea ushindi wa timu ya Ujerumani kwa shangwe kuu
Shangwe na vigelegele vimeshuhudiwa huku umati mkubwa wa watu ukitarajiwa kushuhudia kombe hilo ambalo litapitishwa mjini kote.
Watu wengi wamenunua jezi zenye nyota nne kuashiria ushindi wa nne wa nchi hiyo katika kombe la dunia.

Mashabiki wamepoke ushindi kwa shangwe

Wachezaji wa timu hiyo ambao huchezea timu ya Bayern Munich pia watapata ukaribisho mkubwa baadaye mjni Munich.
Mwandishi wa BBC Steve Evans ambaye yuko mjini Berlin anasema kuwa watu nusu milioni wanatarajiwa kukutana na wachezaji hao mjini Berlin.

SOURCE: BBC

No comments: