Tuesday, January 15, 2013

WADAU WA SOKA MKOANI MTWARA WATAKIWA KUICHANGIA NDANDA FC


Katika kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi daraja la kwanza, klabu ya soka ya Ndanda fc ya Mkoani Mtwara imedhamiria kwenda kuweka kambi ya kujiandaa na mzunguko wa pili na wa lala salama wa ligi hiyo huko Dar Es salaam, ikiwa ni pamoja na kucheza michezo kadhaa ya kirafiki wakiwa huko.

Mratibu wa klabu hiyo Selemani kachele amesema ili kufanikisha hilo na kuiwezesha timu hiyo kucheza ligi kuu msimu ujao, wadau wa soka wa Mikoa ya Lindi na Mtwra wametakiwa kujitokeza kuichangia timu hiyo yenye maskani yake Mkoani Mtwara.

No comments: