Uchaguzi
wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA)
utafanyika Jumamosi (Januari 19 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu wa TAFCA, Eugene Mwasamaki, mikoa ambayo tayari
imefanya uchaguzi wa viongozi inatakiwa kuwasilisha muhtasari wa mkutano
uliowaingiza madarakani. Muhtasari huo uwasilishwe TAFCA kabla ya
keshokutwa (Januari 17 mwaka huu).
Mkoa
utakaoshindwa kutuma muhtasari ndani ya muda uliotolewa utakosa haki ya
kushiriki katika uchaguzi huo uliovutia wagombea watano. Wagombea hao
ni Oscar Korosso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti),
Michael Bundala (Katibu Mkuu) na Magoma Rugora na Wilfred Kidao
wanaowania ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF).
No comments:
Post a Comment