Friday, September 7, 2012

YANGA WATEMBELEA TBL

 



Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kushoto kabisa) akiwa na baadhi ya viongozi wa vitengo mbalimbali vya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) pamoja na wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu ya Yanga juzi Alhamisi wakati mabigwa hao wa Kombe la Kagame walipotembelea kiwanda cha TBL kilichopi Ilala jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kushoto) akiwa na beki mpya wa timu ya Yanga, Mbuyu Twite (katikati) na Msemaji wa timu hiyo, Louis Sendeu Alhamisi wakati timu hiyo yenye maskani yake katika Mtaa wa Jangwani jijini Dar es Salaam ilipofanya ziara katika kiwanda cha kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Anayeonekana nyuma yao ni kocha wa timu hiyo, Tom Sainfiet.

Caption for Kiwandani na Kiwandani 2
Mfanyakazi katika Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Adolf Ndyeabura (aliyevalia fulana ya Yanga kulia) akiwaonyesha kocha wa timu ya Yanga, Thom Sainfiet, na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo jinsi bia zinavyopikwa juzi Alhamisi wakati timu hiyo yenye maskani yake katika mtaa wa Jangwani jijini, ilipofanya ziara yake katika kiwanda cha TBL kilichopo Ilala jijini Dar es Salaam.


YANGA ya Dar es Salaam yenye maskani yake katika Mtaa wa Jangwani Jijini Dar es Salaam leo imefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha kampuni ya bia (Tanzania Breweries Limited – TBL) kilichopo Ilala jijini.
Akiongea katika ziara hiyo afisa habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema timu yake imeamua kufanya ziara yao katika kiwanda hicho ili kuweza kujionea mambo mbalimbali ambayo yanafanywa na kampuni hiyo inayozalisha vinwaji mbali mbali pamoja na bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ndio wadhamini wakuu wa timu hiyo.
Alisema kuwa Kilimanjaro Premium Lager imekuwa ikiwapa ushirikiano mkubwa katika mambo mbalimbali ya kimichezo ikiwa ni pamoja na kuwapatia magari ya usafiri jezi pamoja na vifaa mbalimbali vya michezo hivyo wamefurahishwa sana na jinsi walivyopokelewa vizuri kiwandani hapo na aliwaomba waendelee na moyo huo huo wa kuthamini timu yao.
“Tunawaomba muendele na moyo huo huo kwani sisi kama Yanga, tunaamini kuwa huwezi kutenganisha mafanyikio ya Yanga na udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager na kwamba kwa pamoja, tutaweza kulifikisha soka la Tanzania katika kilele cha ubora,” alisema Sendeu.
Awali, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema kuwa wamefurahishwa sana na kitendo hiki cha timu hii ya Yanga kuamua kuacha shughuli zao na kutembelea kiwanda chao na kujionea kazi za uzalishaji zinavyofanywa kiwandani hapo.
Alisema kuwa Kilimanjaro Premium Lager inathamini mchango wa timu za Yanga kwa soka la Tanzania na ndio maana imekuwa ikiidhamini timu hio huku akibainisha kuwa wataendela kudhamini timu ya Yanga kwa muda mrefu.
Hivi sasa, thamani ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa timu za Yanga unafikia jumla ya dola za Kimarekani 1.5milioni(Shillingi Bilioni mbili) kwa mwaka kwa kila timu. Pesa hizi hutolewa kwa ajili ya shuhuli mbali mbali kama kusajili wachezaji wapya wenye viwango vya kimataifa, mabasi , vifaa vya michezo na kukiwezesha Mkutano Mkuu wa Mwaka na kuijengea uwezo team ya Yanga.
“Tunafanya hivi tukiwa na nia ya kupeleka soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio… Ni dhahiri kuwa timu ya Yanga imekuwa ikifanyia mambo makubwa kwani imekuwa ikiwapatia vijana mbalimbali ajira kupitia timu yao. Ushirikiano wetu na timu ya Yanga inatokana na ukweli kwamba Yanga ndio kati ya timu zenye wapenzi wengi zaidi hapa nchini….timu ya Yanga pia ndio kati ya timu yenye historia yakipekee hapa nchini na inachangia wachezaji wengi kwenye timu ya Taifa Taifa Stars” alisema.
Aliwasihi wananchi kwa ujumla na haswa washabik wa Yanga kuendelea kuisapoti timu kufuatana na mafanyikio yake kwenye ligi na mchango wake kwenye timu ya Taifa na aliitakia Timu ya Yanga kila la heri kwenye msimu wa 2012/2013.
Kavishe alisema ndoa kati ya Kilimanjaro Premium Lager ni yenye mafanikio kwani ndani ya Udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager, timu hiyo imejipatia ubingwa katika mashindano mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata mwaliko kutoka Ikulu ya Tanzania na ile ya Rwanda baada ya kushinda ubingwa wa michuano ya Kagame kwa misimu miwili mfululizo
 
 
 
 
 
 
SOURCE:BIN ZUBEIRY
 
 
 

No comments: