Sunday, April 8, 2012

AC MILAN YAPIGWA NA VIBONDE, INTER YATOA SARE

Ibra
AC Milan iliruhusu nyavu zake kutikiswa dakika ya 90 na mshambuliaji wa Fiorentina, Amauri hivyo kujikuta ikilala 2-1 nyumbani leo na kujiongezea maumivu baada ya kutolewa na Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, siku nne zilizopita.
Kipigo hicho kinaifanya Milan ibaki inaizidi pointi mbili tu Juventus kileleni mwa Serie A, na wanawapa Kibibi Kizee cha Turin nafasi ya kuongzoa ligi iwapo wataifunga Palermo baadaye.
Milan ilipata bao la kuongoza kwa mkwaju wa penalti wa Zlatan Ibrahimovic dakika ya 31 kwenye Uwanja wa San Siro, lakini Stevan Jovetic akasawazisha dakika ya 47.
Nayo Inter Milan imetoka sare ya 2-2 na Cagliari iliyomaliza mechi na wachezaji 10, hiyo ikiwa mechi ya pili chini ya kocha wao mpya, Andrea Stramaccioni.
Katika mechi hiyo iliyocheza huko Trieste, kwa sababu ya mgogoro wa Cagliari na Halmashauri ya Jiji lao juu ya ukarabati wa Uwanja wa Sant’Elia, Davide Astori aliifungia bao la kuongoza Cagliari kwa tik tak dakika ya tano na Diego Milito akasawazisha dakika moja baadaye.
Mshambuliaji wa Chile, Mauricio Pinilla aliifungia la pili Cagliari dakika ya 61 kisha akaonyeshwa kwa ushangiliaji wake na Esteban Cambiasso akasawazishia Inter tena dakika tatu baadaye.
Nayo, Udinese iliifunga Parma 3-1 na kuifikia Lazio katika nafasi ya tatu. Mshambuliaji wa Ghana, Kwadwo Asamoah alifunga mabao mawili kwa Udinese na Antonio Di Natale pia alifunga bao lake la 20 msimu huu.
Lazio inamenyana na Napoli inayoshika nafasi ya tano baadaye.
Roma imefungwa 4-2 na Lecce, Chievo Verona imeifunga Catania 3-2; Bologna imetoka 0-0 na Cesena; na Novara imetoka 1-1 na Genoa.
Mechi zote 10 za Ligi ya Italia zinachezwa leo kwa sababu kesho ni sikukuu ya Pasaka.

No comments: