Juma Mohamed, Juma News
Ndanda FC ya
mkoani hapa imefanikiwa kumaliza vizuri mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya
Vodacom Tanzania Bara baada ya hii leo kusambaratisha Stand United ya Shinyanga
kwa mabao 2-1 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Mabao ya
Ndanda yamefungwa kipindi cha kwanza na Riphati Khamis kwa mkwaju wa penalty
dakika ya 30 baada ya kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari na golikipa wa
Stand Muwonge Frank, huku Ahmad Msumi akifunga la pili kwa kichwa akiunganisha
kona ya Kigi Makassy dakika 45.
Wachezaji wa Ndanda FC walivyofunga bao la pili langoni mwa Stand United, katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara. Ndanda walishinda bao 2-1. |
Stand
walipata bao la kufutia machozi kipindi cha pili baada ya mlinzi wa Ndanda
Bakari Mtama kuusindikiza wavuni mpira uliopigwa na Khamis Frank wa Stand.
Ndanda
wanamaliza mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo wakiwa wamejikusanyia jumla ya alama
19 baada ya mchezo huo, huku Stand United wakiwa na alama 22.Kikosi cha Ndanda FC kilichoanza katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Stand United katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara. Ndanda walishinda bao 2-1. |
Kikosi cha Stand United kilichoanza katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara. Ndanda walishinda bao 2-1. |
No comments:
Post a Comment