Wednesday, November 9, 2016

Madiwani Mtwara washindwa 'kumng'oa' Meya wa Manispaa


Wajumbe wa kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya Mtwara Mikindani, wakiwa katika kikao maalumu cha kujadili ajenda ya kutokuwa na imani na Meya wa manispaa hiyo, Godfrey Mwanichisye.



Naibu Meya wa manispaa ya Mtwara Mikindani, Erick Mkapa akieleza jambo  katika kikao maalumu cha kujadili ajenda ya kutokuwa na imani na Meya wa manispaa hiyo, Godfrey Mwanichisye.


Juma Mohamed, Juma News

Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Mtwara Mikindani kilichokuwa na ajenda ya kutokuwa naimani na mstaiki Meya wa manispaa hiyo, Godfrey Mwanchisye, kimeshindwa kufikia lengo na baadala yake wajumbe kujikuta wanalazimika kuridhia Meya huyo aendelee katika nafasi yake.
Awali wajumbe wa kikao hicho walionekana kushinikiza kuondolewa kwa Meya huyo na kuungwa mkono na naibu Meya ambaye ndio alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho, Erick Mkapa.
Mwanasheria wa Manispaa hiyo, Sifaeli Kulanga, amepingana na matakwa ya wajumbe hao kwa madai kuwa yanakwenda kinyume na taarifa ya tume iliyoundwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara kuchunguza tuhuma zinazomkabili Meya huyo.

Mkurugenzi wa manispaa ya Mtwara Mikindani, Beatrice Diminic akifafanua jambo katika kikao cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo.



Baada ya mijadala hiyo baina ya wajumbe na mwanasheria akiungwa mkono na mkurugenzi wa manispaa Beatrice Diminic, naibu Meya akawasihi wajumbe waridhie hoja za mwanasheria, huku Meya akishukuru kutokana na maamuzi ya kumuacha katika nafasi yake.

No comments: