Msafara wa madereva Bodaboda wilayani Tandahimba ukiongozwa na askari wa usalama Barabarani kuelekea katika kituo cha polisi kwa ajili ya sherehe ya wahitimu wa mafunzo ya usalama barabarani. |
Katibu tawala wa wilaya ya Tandahimba, Azizi Fakhii akimkabidhi zawadi ya shuka kamanda wa polisi wilaya ya Tandahimba, Fraterine Tesha iliyotolewa na madereva Bodaboda |
Juma
Mohamed, Juma News
Baadhi ya
wanawake wanaoendesha pikipiki za abiria maarufu Bodaboda wilayani Tandahimba
mkoani Mtwara wamesema wameamua kuingia katika biashara hiyo kutokana na hofu
ya kupata ajali pindi wanapopakizwa na madereva wanaume kutokana na kuendesha
kwa mwendo kasi.
Msafara wa madereva Bodaboda wilayani Tandahimba ukiongozwa na askari wa usalama Barabarani kuelekea katika kituo cha polisi kwa ajili ya sherehe ya wahitimu wa mafunzo ya usalama barabarani. |
Wakizungumza
wilayani humo badaa ya kuhitimu mafunzo ya elimu ya usalama barabarani
yaliyoendeshwa na chuo cha Apec, wanawake hao walisema hatua hiyo ni njia
mojawapo ya kujiingizia kipato hali ambayo inawafanya kuacha kuwa tegemezi kwa
waume zao.
Katibu tawala wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, Azizi Fakhii akifurahia zawadi ya shuka aliyopewa na mmoja wa madereva Bodaboda wilayani humo. |
Mkuu wa
kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Mtwara, Meloe Buzema, alisema pikipiki
zinachangia asilimia 28 ya ajali zote za barabarani huku katibu tawala wa
wilaya ya Tandahimba Azizi Fakhii akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo
Sebastian Waryuba akawataka washiriki wa mafunzo hayo kuanzisha vikundi kwa
ajili ya kujiunga na SACOS.
Jumla ya
madereva bodaboda 410 wamehitimu mafunzo hayo na kutunukiwa vyeti huku
wakiahidiwa kuondolewa vikwazo katika kuwapatia leseni.
No comments:
Post a Comment