Na
Mwandishi wetu, Juma News
Zikiwa zimebakia
siku 15 kwa promosheni ya”Kamata Mpunga”kuisha na mshindi mmoja wa droo
ya mwisho atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 100. Leo hii mkazi wa
Moshi mjini Hassan Ochieng amejinyakulia kitita cha shilingi milioni 20/= na
Mkazi wa singida mjini ambaye ni muuza mitumba Bw. Aman Manyenye amejinyakulia
kitita cha shilingi Milioni 5/= pamoja na Joseph Machima,Mkazi wa Sengerema
Mkoa wa Mwanza.
“Meneja Uhusiano
wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ametoa wito kwa wateja wa kampuni hiyo na
watanzania wote kwa ujumla ambao hawajajiunga na mtandao huo waweze kujiunga na
kuchangamkia frusa hii yakipekee kabisa kwani kila siku kuanzia Jumatatu hadi
Jumamosi kuna washindi 3 ambapo kila mshindi anajinyakulia shilingi Milioni 1/-
na kila mwisho wa wiki yaani Jumapili kuna mshindi mmoja wa Milioni 5/= na
mwisho wa mwezi kuna mshindi wa milioni 20/= na kuna mshindi wa zawadi kubwa ya
mwisho wa promosheni ni ya kitita cha shilingi Milioni 100/=
Ili mteja aweze
kushiriki katika promosheni hii ni rahisi sana mteja anachotakiwa kufanya ni
kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuandika neno “GO” kwenda namba 15544
ambapo atapata ujumbe wa kumfahamisha kuwa ameingia kwenye mchezo na ataanza
kupokea maswali atakayotakiwa kuyajibu kwa ajili ya kujiongezea pointi za
ushindi na mteja atakatwa shilingi 300 tu kwenye muda wake wa maongezi ”.
maswali
atakayopokea mteja yatakuwa na majibu 2 moja likiwa jibu sahihi na lingine
likiwa sio sahihi.
Kuna wateja
wengine hawana nafasi ya kujibu maswali ili wasipitwe na promosheni hii
wanatakiwa kutuma neno “WIN” kwenda namba 15544 na atakatwa kiasi
cha shilingi 200 tu watakuwa hawahangaiki kujibu maswali ila watakuwa
wameingizwa kwa droo moja kwa moja.
v Mpaka sasa jumla ya washindi 327 wamejinyakulia fedha
mbalimbali tangu kuanza kwa promosheni hii.
v Washindi 297 wamejishindia Milioni mojamoja kila mmoja
v Washindi 18 wa wiki wamejishindia shilingi Milion 5/5
kila mmoja
v Pia washindi 4 wameondoka na kitita cha
shilingi Milioni 20/-
No comments:
Post a Comment