Baadhi wa wakulima wa korosho wa halmashauri ya mji wa Nanyamba, Mtwara wakifuatilia mnada wa ununuzi wa zao hilo. |
Juma Mohamed, Mtwara
Baadhi ya
wakulima wa zao la korosho katika halmashauri ya mji wa Nanyamba mkoani Mtwara,
wameahidi kuongeza kasi ya kufunga ndoa ikiwa ni sehemu ya matumizi ya pesa
wanazozipata kupitia mauzo ya zao hilo
Wakizungumza
na Juma News nje ya ghala la chama cha
msingi cha Dinyecha baada ya kufanyika kwa mnada wa ununuzi wa korosho,
wamesema kupanda kwa bei ya zao hilo kutachangia ongezeko la ndoa holela
maarufu kama Ndoa za Msimu.
“Mimi nasema
nashukuru kwa bei ya korosho…hii bei ya korosho itatufanya sisi wakulima
wadogowadogo sisi kwanza tuwe na fursa ya kupata hela nyingi na kutusaidia
mambo ya Ndoa, tutaoa wanawake tutafanya shughuli zile za kilimo..kwahiyo na
ndoa zenyewe kama zilikua kwa mwaka zinakua 10 au 20 na zaidi na mpaka hata
50..tunamuomba tu rahisi ili aliweke kipaumbele..” alisema Said Ngalile mkazi
wa Nanyamba.
Baadhi wa wakulima wa korosho wa halmashauri ya mji wa Nanyamba, Mtwara wakifuatilia mnada wa ununuzi wa zao hilo. |
Said
Selemani anasema ndoa hizo hupatikana zaidi msimu wa mauzo ya korosho kutokana
na wakulima wengi kupata pesa na kwamba katika msimu huu ambao korosho
inaonekana kuwa na bei nzuri ndoa hizo zitakuwa kwa wingi zaidi.
Asha Salum,
anaeleza namna ndoa hizo zilivyokithiri katika halmashari hiyo pamoja na
kueleza athari ambazo wanawake wanazipata baada ya kuachika kutoka kwa waume
zao.
“Tunatelekezwa
sana sisi akina mama katika ndoa hizo, kwasababu anakuachia familia unahangaika
sana na inakuwa hata watoto hawajali..msimu huu korosho ziko juu sana kwahiyo
nategemea hizi ndoa zitakuwa nyingi sana kwasababu pesa zitakuwepo.” Alisema Asha
Salum
Meneja mkuu
wa chama kikuu cha ushirika cha Mtwara, Masasi Co operative Union MAMCU Kelvin
Rajabu, anaeleza namna minada ilivyofanyika na kampuni zilizoshinda ununuzi.
“Wakulima wa
Masasi wameuza korosho zao kwa bei ya chini ya shilingi 3,760 na bei ya juu ni
3,805 lakini kwa upande wa wakulima wa Mtwara kwa upande wa ghala la Olam
kampuni ya B Southern Trading imeweza kuchukua korosho kwa bei ya 3, 805
japokua ni tani chache tani 230..” alisema
Naye mkuu wa
mkoa wa Mtwara Halima Dendego anawakumbusha wakulima matumizi bora ya fedha
wanazozipata baada ya mauzo, huku akisisitiza wajiwekee akiba kwa ajili ya ununuzi
wa pembejeo mara baada ya msimu kumalizika.
Ndoa za
msimu zimeshamiri zaidi katika maeneo yanayolimwa korosho kwa wingi mikoa ya
Lindi na Mtwara na hufungwa zaidi wakati huu wa mauzo ya zao hilo na kuachana
mara baada ya wakulima kuishiwa pesa.
No comments:
Post a Comment