Na Juma Mohamed.
JUMLA ya
vyumba Tisa vya madarasa vimeteketea katika shule ya sekondari ya Lindi, kufuatia
kuzuka kwa moto mkubwa ulioanza kuwaka majira ya saa Saba za usiku kutokana na
hitirafu ya umeme.
Kamanda wa
polisi wa mkoa wa Lindi Renata Mzinga, ameiambia Juma
News kwa njia ya simu kuwa, mbali na vyumba hivyo, athari zingine
zilizotokana na moto huo ni kuteketeza matundu 26 ya vyoo, ofisi 4 za walimu
pamoja na vyumba viwili vya maabara za Phizikia na Kemia.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, Renata Mzinga. (PICHA: MTANDAO) |
“Ulianzia kwenye
‘Main switch’..chumba ambacho kina ‘Main Switch’ kwamujibu wa mtoa taarifa za
awali ambaye ni mwalimu wa shule hiyo na kwasababu moto huo pale hakuna namna
ya kuingiza zima moto yale madarasa ya nyuma miundombinu ilizuia kuingiza gari
la zima moto kwahiyo wananchi wakawa wanajitahidi kuuzima kwa kuchota maji hiyo
ikapelekea moto kusambaa..”alisema Kamanda.
Aidha,
alisema hakuna madhara mengine yoyote yaliyojitokeza dhidi ya binaadam na
kwamba bado wanafunzi walikuwa hajaanza kuwasili shuleni hapo kutoka makwao
walikokuwa kwa likizo.
No comments:
Post a Comment