Kaunti moja ya
Kaskazini mashariki mwa Kenya imechukua hatua zisizo za kawaida kulinda
barabara moja iliotiwa lami, kwa kuwavalisha nepi punda wanaotumia
barabara hiyo.
Mikokoteni yote inayofanya kazi Wajir sasa
italazimika kuweka begi nyuma ya wanyama hao ili kuokota kinyesi chao
kwa lengo la kuhakikisha barabara iko safi.
Ni barabara kuu ya
kwanza katika historia ya eneo hilo.Wakenya wameenda katika mitandao ya
kijamii ili kusambaza uvumi vile punda wa Wajir wanapaswa kufuata sheria
hiyo mpya mara moja.
Hii hapa taarifa iliotolewa na serikali ya eneo hilo:
''Tunashukuru
mchango unaoletwa na waendesha mikokoteni ya punda kwa uchumi wa
Wajir,hatahivyo,mji huo ni sharti usafishwe kila mara.Kutokana na
hilo,mumeagizwa kusimamia kinyesi cha punda wenu ili kutochafua
barabara.Hakuna Punda atakayeruhusiwa mjini bila mfuko wa kubebea
kinyesi kufikia tarehe 29 mwezi Mei''.
No comments:
Post a Comment