Kutoka kwenye sare
mbili mfululizo katika mechi za mashindano,timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa
Stars’ chini ya kocha mzalendo Charles Boniface Mkwasa ambaye amekula shavu la uhakika la kuinoa timu hiyo hadi 2017, leo imefanikiwa kuibuka
na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Malawi kwenye mchezo wa awali uliopigwa kwenye
uwanja wa Taifa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka 2018
nchini Urusi.
Iliwachukuwa
dk 19 tu Stars kabla ya kuwainua mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo, kupitia
bao safi la Mbwana Samata akiunganisha pasi ya mchezaji mwenzake wa TP Mazembe
Thomas Ulimwengu.
Mashabiki waliojitokeza kushuhudia pambano kati ya Stars dhidi ya Malawi huku wakiwa mamebeba bango lenye ujumbe wa kumwamini Mkwasa |
Stars
baada ya kupata goli hilo waliamka na kuanza kucheza mpira na kutawala mchezo
kwa asilimia nyingi katika kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi kadhaa za
kufunga lakini nafasi hizo hazikutumiwa ipasavyo kwani bado walipoteza nafasi
nyingi za kufunga.
Dk tatu baadaye, Thomas
Ulimwengu aliiandikia Stars bao la pili kufuatia makosa ya mlinda mlango wa ‘The
Flames’ baada ya kuutema mpira uliopigwa na Haji Mwinyi kasha kumkuta mfungaji na
kuihakikishia timu hiyo kupata ushindi wa kwanza tangu imeanza kunolewa na
Mkwasa aliyepokea kijiti hicho toka kwa kocha Mart Nooij aliyetimuliwa mwezi
Julai mwaka huu.
Kabla
ya mchezo wa leo, Stars ikiwa chini ya kocha Mkwasa imetoka sare kwenye mechi
mbili za mashindano na kupoteza mchezo mmoja wa kirafiki.
Sare ya kwanza
ilikuwa ni dhidi ya Uganda mchezo uliochezwa Uganda kuwania kufuzu kucheza
fainali za Afrika kwa wacheaji wa ligi za ndani (CHAN) huku wakitoka sare ya
bila kufungana dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika.
Stars
ikiwa chini ya Mkwasa ilipoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Libya kwa goli 2-1
wakati ikiwa Uturuki kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria.
SOURCE: SHAFFIH DAUDA
No comments:
Post a Comment