Monday, September 21, 2015

PICHAZ..wakazi wa manispaa ya Mtwara Mikindani wakiwa katika maandalizi na shamrashamra za kumpokea Mhe. Lowassa..wafanyabiashara kufunga maduka..

Na Juma Mohamed

SHUGHULI za kibiashara katika soko kuu la manispaa ya Mtwara Mikindani na maeneo mengine zitasimama kwa muda baada ya wafanyabiashara kusema watakuwa katika mkutano wa mgombea Urais kuptia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Mhe, Edward Lowassa, utakaofanyika muda mfupi ujao katika viwanja vya Mashujaa mkoani hapa.

wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao walisema kutokana na wanunuzi wengi watakuwa katika mkutano huo, wao hawana sababu ya kukaa katika biashara zao kwakuwa hakutakuwa na watu wa kuwauzia, hivyo biashara zitajifunga zenyewe.

Bango la Mhe. Lowassa likiwa limepambwa kwa mashada na kuzungushia wigo wa makuti.


Vijana wa bodaboda maeneo ya nje ya soko kuu la Manispaa ya Mtwara



Maandalizi ya eneo la uwanja wa Mashujaa ambako Mhe. Lowassa anataraji kuhutubia




Vijana wa bodaboda maeneo ya nje ya soko kuu la Manispaa ya Mtwara




Vijana wa bodaboda maeneo ya nje ya soko kuu la Manispaa ya Mtwara



Dereva wa Toyo



Duka linalouzwa bidhaa zenye nembo ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)



Maandalizi: vijana wakiwa katika kuliandaa bango la Mhe. Lowassa ambalo litafungwa kwenye Bajaji.








Bango la Mhe. Lowassa na wagombea ubunge.


No comments: