Monday, September 21, 2015

Lowassa asimamisha biashara Mtwara..watu wafurika Mashujaa kusikiliza sera


Maelfu ya wakazi wa Mtwara waliofurika katika mkutano wa mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia UKAWA, Mhe. Edward Lowassa, uliofanyika leo katika viwanja vya Mashujaa mkoani hapa.






Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Fedrick Sumaye, akihutubia leo mkoani Mtwara katika mkutano wa kunadi sera za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kumnadi mgombea Urais wa chama hicho, Mhe. Edward Lowassa.


Maelfu ya wakazi wa Mtwara waliofurika katika mkutano wa mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia UKAWA, Mhe. Edward Lowassa, uliofanyika leo katika viwanja vya Mashujaa mkoani hapa.



Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia UKAWA, Mhe. Edward Lowassa, akihutubia maelfu ya wakazi wa Mtwara waliofurika katika mktano wa kunadi sera za chama hicho uliofanyika leo katika viwanja vya Mashujaa mkoani hapa.


Maelfu ya wakazi wa Mtwara waliofurika katika mkutano wa mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia UKAWA, Mhe. Edward Lowassa, uliofanyika leo katika viwanja vya Mashujaa mkoani hapa.











Na Juma Mohamed.
Shughuli za kibiashara katika soko kuu la manispaa ya Mtwara Mikindani na maeneo mengine zilisimama kwa muda baada ya wafanyabiashara kuamua kwenda kusikiliza sera za mgombea Urais kuptia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) chini ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Mhe, Edward Lowassa, uliofanyika jana katika viwanja vya Mashujaa mkoani hapa.

wakizungumza kwa nyakati tofauti, wafanyabiashara hao walisema kutokana na wanunuzi wengi kuwa katika mkutano huo, wao hawana sababu ya kukaa katika biashara zao kwakuwa hakutakuwa na watu wa kuwauzia, hivyo biashara zitajifunga zenyewe.
Walisema wamechoshwa na utawala wa chama kimoja na kwamba wanahitaji mabadiliko ambayo wanaimani yatapatikana iwapo Mhe. Lowassa ataingia madarakani kutokana na sera zake kuwa zinatekelezeka.
Kutokana na hali hiyo, mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, alisema kwakuwa ni maamuzi yao wenyewe hakuna sababu ya kuwazuia, hivyo ni matakwa yao kuamua kufunga au kutofunga biashara zao.
“Mtu akifanya hivyo kwa maamuzi yake hakuna tatizo, kwasababu anafunga kwa mapendekezo yake mwenyewe..lakini kama kuna shinikizo kutoka kwa baadhi miongoni mwao, sasa hao ndio wakupaswa kuchukuliwa hatua za kisheria, kwasababu huwezi kumlazimisha mwenzio afanye kitu hasichokipenda..” alisema Dengedo, alipohojiwa na kituo kimoja cha redio mkoani hapa.
Katika mkutano huo, ulioanza majira ya saa kumi nambili kasoro kutoka na hitilafu ya mitambo, Lowassa alisema iwapo atachaguliwa kuwa Rais ataunda tume kwa ajili ya kuchunguza upya mikataba ya gesi na mafuta.

Alisema anafahamu kiu ya wananchi wa Mtwara na namna walivyokerwa juu ya kunufaika na rasilimali hizo, ambazo ni chachu kubwa ya maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Alisema, wakazi wa Mtwara na watanzania kwa ujumla hawapaswi kuwa masikini kutokana na kuwa rasilimali nyingi, na kwamba akiingia madarakani atahakikisha maisha ya kila mwananchi yanapiga hatua za kimaendeleo katika kila nyanja.
“Kama mkinichagua, kila mtanzania kama alikuwa anakula milo miwili basi itaongezeka na kuwa mitatu, na kama anamiliki gari moja basi atamiliki magari mawili..nataka kuwa Rais wa nchi hii kwasababu nimechoshwa na umasikini wa taifa na wananchi wake.” Alisema.
Aidha, Lowassa alitumia nafasi ya kufanya mkutano huo kwa kujaribu kutatua mgogoro wa jimbo la Mtwara mjini ulio kati ya wagombea wa vyama vitatu kati ya vinne vya UKAWA ambavyo ni NCCR-Mageuzi, CHADEMA na CUF, ambapo aliwaita wagombea wote na kuwapa dakika tatu za kujinadi kwa wananchi kisha kuwaahidi kulitolea majibu baada ya muda mfupi kutokana na matakwa yao kwamba wanahitaji mgombea gani.
Kati ya wahgombea wawili wanaogombea jimbo hilo waliojinadi ambao ni Joel Nanauka (CHADEMA) na Maftah Nachuma (CUF), wananchi walionekana kumkubali zaidi Nachuma, ambapo Lowassa aliwaahidi kwamba maamuzi yao yataheshimiwa na hayatabadilika.

Kwa upande wake, waziri mkuu mstahafu wa serikali ya awamu ya tatu, Mhe. Fedrick Sumaye, alimtaka mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. John Magufuli, kuhamia UKAWA na kuungana na Lowassa, kwasababu anaonyesha kunogewa na sera na misemo ya CHADEMA.
“Tunamuambia Magufuli, kama amechoka kuwa na  CCM basi alete kadi yake hapa kwa Mhe. Lowassa na ajiunge nasi kwasababu anaonekana ameishiwa sera..maana hata misemo yetu anaichuku, kwamfano M4C anasema Magufuli For Change..” alisema.
Aliwasisitiza wananchi kutokuwa waoga katika kufanya mabadiliko kwa kuhofia kutokewa kwa vurugu, akitolea mfano nchini Libya ambako kulitokea vurugu kwa ajili ya kuipinga serikali ya Muammar Ghadaf, na kusema vurugu hizo zilitokana na serikali hiyo kung’ang’ania madaraka kama ilivyo kwa CCM.

No comments: