Mario Balotelli |
Mchezaji 'mtukutu' wa Liverpool Mario Balotelli atarejea AC Milan kwa mkopo wa msimu mmoja baada ya klabu hizo mbili kuafikiana kuhusu mkataba wa mkopo hii leo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia ameshuka sana tangu ajiunge na klabu hiyo ya Ligi ya Premia baada ya Kombe la Dunia mwaka jana na hajachezea Italia tangu wakati huo.
Lakini huku mechi za Ubingwa Ulaya zikitarajiwa kuanza Ufaransa majira yajayo ya joto, mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 25 anatarajiwa kurejea klabu aliyoihama mwaka mmoja tu uliopita.
Ripoti kwenye tovuti ya Gazzetta dello Sport ilisema Balotelli atafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika uwanja wa mazoezi wa Milan wa Milanello Jumanne.
Yote yakienda sawa, huenda akawa tayari kuchezea Milan mechi yao ya kwanza nyumbani msimu huu dhidi ya Empoli.
Habari hizo ziliongeza kwamba hakuna kifungu kinachowapa Milan uhuru wa kumnunua Balotelli moja kwa moja mwisho wa msimu.
Wengi wa mashabiki wa Milan, hata hivyo, wanaonekana kutofurahia kurejea kwa Balotelli.
Kwenye kura ya maoni kwenye tovuti ya Gazzetta wiki iliyopita, asilimia 74 ya wasomaji waliamini ni “hatua isiyofaa” kwa klabu hiyo, asilimia 26 pekee ya wasomaji wakiwa ndio waliofurahia hatua hiyo.
Hata hivyo, wakuu wa klabu hiyo akiwemo Afisa Mkuu Mtendaji Adriano Galliani, wamekuwa wakishinikiza kurejea kwake.
Balotelli alianza uchezaji wake soka ya kulipwa chini ya Roberto Mancini Inter Milan, kocha wa sasa wa Milan Milan Sinisa Mihajlovic alipokuwa msaidizi wa kocha huyo, 2007.
Alikaa miaka mitatu ya misukosuko Manchester City kuanzia 2010 hadi 2013, kipindi alichojihusisha katika sarakasi nje ya uwanja na utovu wa nidhamu uliopelekea kukosana kwake na kocha wa City wakati huo Roberto Mancini.
Balotelli alirejea Italia, akijiunga na mahasimu wakuu wa Inter, AC Milan Januari 2013 lakini akauzwa Liverpool 2014.
SOURCE: SUPER SPORT
No comments:
Post a Comment