Thursday, July 23, 2015

Wanasiasa Mtwara watakiwa kuacha kuzungumzia Bomba la Gesi


Mratibu wa shirika la Faidika Wote Pamoja (FAWOPA), Bartazar Komba, akifunga mkutano wa ufunguzi wa mradi wa Pamoja Tunufaike na Rasilimali Zetu jana katika ukumbi wa Bandari Klabu.

Wajumbe wa mkutano wa ufunguzi wa mradi wa Pamoja Tunufaike na Rasilimali Zetu, uliofanyika jana katika ukumbi wa Bandari Klabu.


Msaidizi wa mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu  (UNESCO) nchini Tanzania, Joel Nanauka, akifafanua jambo kuhusu sekta ya mafuta na gesi.


 Na Juma Mohamed, Mtwara
 
WANASIASA mkoani Mtwara wametakiwa kuacha kuzungumzia swala la ujenzi wa bomba la gesi asilia linalotoka Madimba mokani hapa mpaka Dar es Salaam, kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi na baadala yake wajikite katika kutetea ajira kwa vijana.

Hayo yalizungumzwa jana mjini hapa na mratibu wa shirika la Faidika Wote Pamoja (FAWOPA) Bartazar Komba, wakati wa kufunga mkutano wa ufunguzi wa mradi wa Pamoja Tunufaike na Rasilimali Zetu, katika ukumbi wa Bandari klabu.



Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma S. Ally, akifungua mkutano wa ufunguzi wa mradi wa Pamoja Tunufaike na Rasilimali Zetu.


Alisema swala la kuzungumzia bomba la gesi kwa sasa halina maana na ni sawa na kupoteza muda kwani tayari ujenzi umeshakamilika na gesi itasafirishwa, hivyo ni wakati wa kuangalia changamoto zingine ambazo wananchi wanakabiliana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira.

Wajumbe wa mkutano wa ufunguzi wa mradi wa Pamoja Tunufaike na Rasilimali Zetu, wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya Mtwara, Fatma S. Ally.




“Wanasiasa tunapoenda kwenye uchaguzi, tuzungumzie zaidi mambo ya ajira na fursa na tuache mambo ya bomba..mambo ya bomba yatatuletea shida, sintofahamu na tutawachanganya wananchi, bomba limekwisha jengwa sasa na linaenda hatuwezi kurudi nyuma..lazima tufanye kazi yenye matunda jamani..” alisistiza Komba.

........................................mwisho.............................

No comments: