Na Juma Mohamed
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) itaanza Sept 12 badala ya Agosti
22 ili kumpa Charles Mkwasa fursa ya kuendelea na program yake kuelekea mechi
ya Taifa Stars vs Nigeria itakayochezwa Sept 5.
Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) itakayozikutanisha
Azam FC dhidi ya Yanga SC sasa itachezwa Agosti 22 badala ya Agosti 15.
Ratiba ya Ligi Kuu iliyokuwa imeandaliwa, sasa inafanyiwa
marekebisho kwa ajili ya tarehe mpya ya kuanza, ambapo pamoja na mambo mengine
mechi sasa zitachezwa wikiendi na katikati ya wiki na wikiendi ya Oct 25
hakutakuwa na mechi kupisha Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge.
Klabu za Ligi Kuu zimeandikiwa barua kujulishwa tarehe mpya ya
kuanza Ligi, na dirisha la usajili linabaki kama lilivyo.
Wamiliki wa viwanja vyenye upungufu wmeandikiwa barua kutakiwa
kurekebisha upungufu katika muda maalumu, vinginevyo havitaruhusiwa kutumika
kwa ajili ya PL na FDL.
Timu ya Madini ya Arusha imeruhusiwa kutumia Uwanja wa Nyerere
uliopo Mbulu mkoani Manyara kwa mechi za SDL kwa masharti upungufu uliopo
kwenye uwanja huo urekebishwe kwanza.
SOURCE: TFF
No comments:
Post a Comment