Na Juma Mohamed
Timu
ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania wenye umri chini ya miaka 20 (Tanzanite)
wanatarajiwa kuondoka kesho jumatano asubuhi kwa Rwanda Air kuelekea nchini
Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Young She-Polopolo.
Tanzanite
inayowania kufuzu kwa Fainali za Kombe Duniwa mwaka 2016 nchini Papua New
Guinea, itacheza mchezo huo wa marudano siku ya jumamosi tarehe 25 Julai, jijini
Lusaka.
Katika
mchezo wa awali uliofanyika takribani wiki mbili zilizopita, Tanzanite
ilipoteza mchezo wake nyumbani baada ya kufungwa kwa mabao 4 – 0, hivyo
kuhitaji kushinda zaidi ya mabao 5 – 0 ili kuweza kusonga katika hatua
inayofuata.
Msafara
wa Tanzanite utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Blassy Kiondo
utajumuisha makocha Rogasian Kaijage (kocha mkuu), Edna Lema (kocha msaidizi),
Peter Manyika (kocha wa makipa), Christina Luambano (Daktari), Mwanahamis
Abdallah (mtunza vifaa) na Meneja Furaha Francis.
Wachezaji
watakaosafiri ni Stumai Abdallah, Shelder Boniface, Donisia Minja, Najiat
Abbas, Neema Kiniga, Happyness Mwaipaja, Jane Lucas, Anastazia Katunzi, Anna
Mwaisura, Janet Pangamwene, Gelwa Rugomba, Blandina Ambros, Amina Ramadhan,
Asha Shaban, Maimuna Hamis, Zuwena Hamis, Amisa Athuman na Wema Richard.
SOURCE: TFF
No comments:
Post a Comment