Mshauri wa masuala ya habari na mawasiliano wa Shirika Utangazaji la nchini Uingereza (BBC), Ndimara Tegambwage, akitoa somo kwa waandishi wa habari mkoani Mtwara juu ya kuandika habari za uchaguzi. |
Na Juma Mohamed, Mtwara
Waandishi wa
habari nchini wametakiwa kuwa na ujasiri katika kufanya kazi zao hasa katika
kuandika habari za uchaguzi, ili kupata habari sahihi zisizokuwa na upendeleo
kwa masilahi ya wanasiasa.
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoani Mtwara wakiwa katika mafunzo juu ya kuandika habari za uchaguzi |
Wito huo ulitolewa jana mkoani hapa na mshauri wa masuala ya habari na mawasiliano wa shirika
utangazaji la Uingereza (BBC), Ndimara Tegambwage katika semina kwa waandishi
wa habari kuhusu namna ya kuandika habari za uchaguzi.
Ndimara Tegambwage |
Aidha, amesema
lengo la kutoa semina hiyo ni kuwawezesha waandishi wa habari kuelewa nafasi ya
taaluma yao katika kuandika habari katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea
katika uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais.
…………………………….mwisho………………………………………………
No comments:
Post a Comment