Abdallah Chikota akiwa amekabidhi fomu kwa katibu wa CCM wilaya ya Mtwara vijijini jana Amina Imbo |
Na Mwandishi wetu, Mtwara.
WANANCHI wa
jimbo la Nanyamba, mkoani hapa wameahidiwa neema za kutatuliwa changamoto kubwa
za ukosefu wa maji na mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Abdallah Dadi Chikota iwapo atafanikiwa kuwa mwakilishi wao katika bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza
na NEWS ROOM muda mfupi baada ya kurudisha fomu katika ofisi za CCM wilaya ya
Mtwara vijijini, Chikota alisema Hawa Ghasia amejitahidi kutatua baadhi ya
changamoto zilizopo jimboni humo lakini zipo ambazo bado zinahitaji kufanyiwa
kazi ikiwa ni pamoja na kero ya maji ambayo imekuwa ni ya muda mrefu.
Wanachama wa CCM waliojitokeza kumsindikiza Abdallah Chikota wakati anarudisha fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Nanyamba jana |
“Changamoto
ya kwanza ambayo ipo katika maeneo yetu ni swala la maji..tuna miradi mikubwa
sana ya vijiji kumi ambayo imeandikwa katika kila halmashauri, lakini miradi
hii bado haijaweza kutatua changamoto hii na kama tunavyofahamu kuwa eneo letu
lipo chini ya mradi mkubwa ule wa makonde lakini bado tuna shida kubwa sana ya
maji..kwahiyo kipaumbele changu cha kwanza ni kuhakikisha tunashirikiana na
wananchi na serikali katika kipindi hiki cha miaka mitano tunalipunguza na kama
sio kulimaliza kabisa..” alisema.
Naye katibu
wa CCM wilaya ya Mtwara vijijini, Amina Imbo, aliwataka wanachama wa chama
hicho kuwa na umoja na wale watakao kosa nafasi ya kupitishwa katika mchujo
kuwa wagombea, kutokuwa na tabia ya kuwaunga mkono wapinzani au kuwavunja moyo
wale waliopitishwa.
Abdallah Chikota akikabidhi fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Nanyamba kwa katibu wa CCM wilaya ya Mtwara vijijini, Amina Imbo |
Aidha,
aliwataja waliochukuwa fomu za ubunge mpka juzi saa 8 mchana kwa jimbo la
Mtwara vijijini kuwa ni mbunge aliemaliza muda wake na waziri wa Tamisemi, Mhe.
Hawa Ghasia na Selemani Libubulu huku jimbo jipya la Nanyamba ni Abdallah
Chikota na Selemani Livanga.
…………………………………….MWISHO……………………………………………..
No comments:
Post a Comment