Sunday, July 19, 2015

Mwameja asisitiza nidhamu kwa magolikipa wa Tz


Mohammed Mwameja



Na Juma Mohamed.
Golikipa mahiri wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Tanzania Mohamedi Mwameja amewataka magolikipa kujituma na kuzingatia nidhamu kwenye fani hiyo ili kufikia mafanikio.
Mwameja ambaye alipewa jina la ‘Tanzania One’ kwa umahiri wake wa kusimama imara langoni amekiri kuwa kuna magolikipa wengi wa sasa ambao hawajitumi kama ipasavyo na hivyo kuleta mafanikio kwenye klabu zao na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na simbasports.co.tz amesema nidhamu na kujituma ndio siri ya mafanikio yake alioyapata wakati akiwa Simba. “Nafasi hii ya kuwa mlinda mlango inahitaji umakini wa hali ya juu sana, kujituma na nidhamu jambo ambalo mpaka sasa bado walinda mlango wengi wanakosa sifa na tunu hizo muhimu katika soka”.
Kwa upande mwingine Mwameja ambaye anashiriki mafunzo ya Makocha wa makipa ya FIFA yanayofanyika uwanja wa Karume yalioandaliwa na TFF, ameushukuru uongozi wa Simba kwa kutambua umuhimu wake na kumuwezesha kushiriki kozi hiyo ambayo kwa mara ya kwanza inafanyika hapa Tamzania.
 “Unajua ujuzi hauozi, mafunzo ninayoyapata hapa kwa hakika yananiongezea uwezo mkubwa sana tofauti na uzoefu wangu na kufanya kazi kwa mazoea. Kwakweli Simba naishukuru sana kwa maamuzi yake haya ya busara ya kuniwezesha kushiriki mafunzo haya yanayofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania. Mimi ni mtu ninae amini sana kwenye kujenaga urithi kwa vijana na naamini kuwa ujuzi nitakaoendelea kuupata hapa nitautumia kujenga magolikipa imara wa nchi hii” alisema Mwameja.
Mwameja alizaliwa Desemba 21, mwaka 1964 katika eneo la Mwakidila mkoani Tanga, na alichezea timu ya Simba na Taifa kwenye nafasi ya ugolikipa.
Mafuzo hayo yanashirikisha jumla ya makocha 31 wa makipa kwenye vilabu vyote vya ligi kuu Tanzania na Simba imemuwezesha Mwameja kushiriki.

SOURCE: Simbasports.co.tz

No comments: