Hatua
ya Robo Fainali ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame
Cup 2015) inatarajiwa kuendelea leo Jumatano kwa michezo miwili kuchezwa katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku macho na masikio yakiwa kwenye
mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC.
Mechi hiyo ya pili ambayo itaanza saa
10:15 jioni inatarajiwa kuwa ya vuta nikuvute kufuatia timu hizo mbili
zinatotokea jijini Dar es salaam kuwa na upinzani mkali kuanzia katika Ligi Kuu
a Vodacom Tanzania na michuano mingine.
Kocha
mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema hana cha kuogopa katika mchezo huo dhidi
ya Yanga, vijana wake amewandaa kupambana katika hatua hiyo ya robo fainali na
ana imani wataibuka na ushindi.
Stewart
ameongeza kuwa ana wigo mpana wa kikosi chake, katika hatua ya makundi wameweza
kushinda michezo yao yote mitatu na kufunga mabao 8, huku ukuta wake ukiwa
haujaruhusu bao hata moja kuingia wavuni kwake.
Kwa
upande wa Yanga, kocha Hans Van der Pluijm amesema naaiheshimu klabu ya Azam,
na katika mchezo huo hana cha kupoteza, kikosi chake kimehimalika kila idara
kuelekea katika hatua ya robo fainali.
Hans
anajivunia kikosi chake ambacho kimeonyesha mabadiliko makubwa kutoka mchezo
wake wa awali iliyoupoteza, na kushinda michezo mitatu mfululizo iliyofuatia
katika hatua ya makundi.
Mchezo
wa kwanza wa robo fainali utazikutanisha timu za KCCA ya Uganda dhidi ya Al
Shandy ya Sudan, mechi itakayoanza saa 7:45 mchana uwnaja wa Taifa jijini Dar
es aalaam.
Wakati
huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB nchini Tanzania Ineke Bussemaker
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa robo fainali kati ya Azam FC
dhidi ya Yanga SC.
AZAM LEO
Manula Aishi
Agrey Morris
Kheri Abdallah
Pascal Wawa
AZAM LEO
Manula Aishi
Agrey Morris
Kheri Abdallah
Pascal Wawa
Shomari Kapombe
Farid Mussa Shah
Himid Mao Mkamy
Jean Mugiraneza
Domayo Frank
John Bocco
Kipre Cheche
Sub
1.Mwadini Ali
2.Metacha Mnatha
3.Said Morald
4.Ammy Ali
5.Abbas Mudathir
6.Didier Kavumbagu
7.Gadiel Michael
Hiyo ndio lineup ya leo .
Farid Mussa Shah
Himid Mao Mkamy
Jean Mugiraneza
Domayo Frank
John Bocco
Kipre Cheche
Sub
1.Mwadini Ali
2.Metacha Mnatha
3.Said Morald
4.Ammy Ali
5.Abbas Mudathir
6.Didier Kavumbagu
7.Gadiel Michael
Hiyo ndio lineup ya leo .
RAIS
WA FFB KUWASILI LEO
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Burundi (FFB), Reverien Ndikuriyo amewasili
jana saa 5 usiku jijini Dar es salaam kwa shirika la Ndege la Rwanda Air.
Ndikuriyo
anatarjaiwa kuwa na mazungumzo na Rais wa TFF, Jamali Malinzi kisha atashuhudia
michuano ya kombe la Kagame inayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es salaam
ikiwa katika hatua ya robo fainali kwa sasa.
Aidha
Vicent Nzamwita Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Rwanda (FERWAFA)
anatarajiwa kuwasili nchini alhamis akiambatana na kocha wa timu ya Taifa ya
Rwanda (Amavubi) John McKinstry.
Rais
huyo baada ya mazungumzo hayo na Jamal Malinzi, baadae kuhudhuria michuano ya
Kombe la Kagame inayoendelea nchini Tanzania.
SOURCE:
TFF
No comments:
Post a Comment