Tuesday, July 21, 2015

Coastal Union wataja waliosajiliwa msimu huu, wapo kutoka Ndanda Sc na Stand United


Na Juma Mohamed
KLABU ya Coastal Union imeweza kusajili wachezaji 13 ambao wataitumikia timu hiyo katika michuano ya Ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba mwaka huu hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,Ofisa Habari wa klabu hiyo,Oscar Assenga alisema kuwa wachezaji ambao wamesajiliwa wametoka timu mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.

Aliwataja wachezaji hao kuwa ni Abasalim Chidebele ambaye ni mshambuliaji kutoka timu ya Stand United ya Shinyanga, Kiungo Mkabaji Adeyum Salehe kutoka JKU ya Zanzibar,Kiungo Mshambuliaji Nasoro Kapama na Beki wa kati Ernest Mwalupani kutoka Ndanda FC ya Mtwara.

Wengine ni Beki wa Kushoto ,Yassin Mustapa Salim kutoka Stand United,Kiungo Sultan Juma kutoka klabu ya African Sports,Mshambuliaji Ahmde Shiboli kutoka Klabu ya African Sports,Mohamed Hamis Mititi ambaye ni mchezaji huru.
Aidha, alisema wachezaji wengine ni Benedict Haule ambaye alisajiliwa akiwa kama mchezaji huru ambaye ni mlinda mlango,Mshambuliaji Ismail  Mohamed Suma kutoka Stand United, winga wa kushoto ambaye ni mchezaji huru Patrick Protas Kamuhagile.

 wengine ni Jackson Sabweto ambaye ni Mlinda Mlango kutoka Klabu ya VILLA FC ya nchini Uganda amesaini mkataba wa miaka miwili,Yossouph Sabo kutoka Klabu ya Younde FC ya Cameroon ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja.

Alisema wachezaji wa zamani waliobaki kutimukia klabu hiyo ni Bakari Mbwana “Kibacha”,Abdallah Mfuko,Hamadi Juma,Ibrahim Chuma,Ike Bright Obina,Abdulhalim Humud,Godfrey Wambura,Ayoub Semtawa na Sued Tumba.
Wakati huo huo wachezaji watano wamepandishwa na uongozi wa Coastal Union  kutoka timu ya vijana   kutokana na uwezo wao kuwa mzuri na wa kuridhisha.
Waliopandishwa ni Mohamed Shekuwe,Sabri Sabri,Tumaini Bakari,Fikirini Suleiman na mtenje Albano

...................................Mwisho...............................

SOURCE: COAST UNION

No comments: