Rais wa China Xi Jinping |
Leo nafurahi sana kuona ukunjufu
zaidi kwa kuweza kukutana na marafiki wote kwenye kituo cha kimataifa cha
mikutano cha mwakalimu Nyerere cha Tanzania.
Katika miaka ya hivi karibuni, chini
ya uongozi wa rais Kikwete, utulivu umedumu katika hali ya kisiasa nchini
Tanzania, mambo ya ujenzi yanaendelea motomoto, yote hayo yamefanya kazi kubwa
katika mambo ya Afrika na mambo ya kimataifa.
Wananchi wa China na Afrika wameunda
hisia za kindugu za kusaidiana na kufanya ushirikiano wa dhati.
Mpaka mwaka jana, vitega uchumi
vilivyowekezwa moja kwa moja na China barani Afrika vimezidi dola za kimarekani
bilioni 15.
Baada ya China kukumbwa na tetemeko
kubwa la ardhi huko Wenchuan, nchi za Afrika zilitoa msaada kwa watu
walioathirika.
Urafiki na ushirikiano kati ya
wananchi wa China na wananchi wa Afrika, umekuwa alama ya uhusiano kati ya
China na Afrika, ambao umesifiwa sana na jumuiya ya kimataifa.
Historia hii imetuambia kuwa, China
na Afrika siku zote ni jumuia ya mustakabali wa pamoja.
Kila upande wetu siku zote una
msimamo wazi na kuunga mkono upande mwingine bila kusitasita katika masuala
yanayohusu maslahi makuu ya upande mwingine.
Historia hii imetuambia, tunapaswa
kwenda na wakati wa kufanya uvumbuzi ili kufanya uhusiano kati ya China na
Afrika uwe na nguvu kubwa ya uhai.
Kusukuma mbele ushirikiano wa China
na afrika ni matumaini ya pamoja ya wananchi wa pande zotu mbili, huu unafuata
mkondo wa duniani, na kuambatana na nia ya wananchi.
Maendeleo ya China hayataweza
kudhoofisha uhusiano wake na Afrika, bali yataimarisha tu uhusiano wake na
Afrika.
Tunawatendea marafiki wa Afrika kwa
udhati. Marafiki wa dhati ni wenye thamani zaidi.
Pande mbalimbali zinapaswa kuheshimu
ustaarabu wa aina mbalimbali duniani na njia mbalimbali za kujiendeleza.
Afrika ni bara la waafrika, nchi
yoyote inayoendeleza uhusiano kati yake na Afrika inapaswa kuheshimu heshima ya
Afrika na juhudi zake za kujiamulia.
China ikitoa ahadi zake, hakika
itatekeleza kihalisi ahadi zake hizo.
Katika miaka mitatu ijayo China
itazisaidia kuwaandaa watu elfu 30 wenye ujuzi wa aina mbalimbali, itatoa
udhamini wa masomo kwa wanafunzi wa Afrika wapatao elfu 18.
China itaendelea kutoa msaada wa
kustahiki kwa maendeleo ya Afrika bila masharti yoyote ya kisiasa.
Msingi na mizizi ya uhusiano kati ya
China na Afrika iko kwa wananchi wa pande mbili.
Na tamthiliya ya China ya
"Doudou na mama wakwe zake" inayooneshwa nchini Tanzania imewafanya
watazamaji wa Tanzania wajihisi ladha za aina mbalimbali za maisha ya familia
za raia wa China.
Tunapaswa kutilia maani zaidi
mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Afrika na kuongeza maelewano na
ufahamu wa wanachi wa pande mbili.
China imejiunga na itaendelea
kujiunga na nchi za Afrika, kuchukua hatua halisi za kushguhulikia vizuri
matatizo yaliyoko kwenye ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na
Afrika.
Daima China itazichukua nchi za
Afrika kuwa marafiki zake wa dhati katika wakati wowote.
Maendeleo ya China hayawezekani
kutengana na dunia na Afrika, na ustawi na utulivu wa dunia na Afrika pia
unaihitaji China.
Wananchi wa China na Afrika
wanatakiwa kuimarisha mshikamano na ushirikiano, ili kujitahidi kutimiza ndoto
ya kila upande.
Tutajiunga na jumuiya ya kimataifa
katika kuhimiza juhudi za kutimiza amani ya kudumu na ustawi wa pamoja, ili
kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya amani na maendeleo ya binadamu.
No comments:
Post a Comment