Uchaguzi
wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake Tanzania (TWFA)
unatarajia kufanyika Desemba 19 mwaka huu mjini Morogoro.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala,
uchaguzi huo utatanguliwa na Mkutano Mkuu wa TWFA. Wajumbe wapiga kura
wote wa mikoa iliyofanya uchaguzi wake na kutoa taarifa za uchaguzi wao
ofisi za TWFA wanatakiwa kufika Morogoro siku moja kabla (Desemba 18
mwaka huu).
Wagombea
waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ni kama ifuatavyo;
wanaowania uenyekiti ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy. Rose
Kissiwa ni mgombea pekee wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Wanaowania
ukatibu mkuu ni Amina Karuma na Cecilia Mkafu. Nafasi ya mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inagombewa
na Zena Chande pekee baada ya Furaha Francis kujitoa kutokana na sababu
za kifamilia.
Sophia Charles na Triphonia Temba wanawania nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho.
Wagombea Rahim Maguza, Macky Mhango na Rose Msamila wameondolewa kwa kushindwa kikidhi matakwa ya Katiba ya TWFA Ibara ya 28(2).
COASTAL YAANZA VIZURI MICHUANO YA KOMBE LA UHAI
Coastal
Union ya Tanga imeanza vizuri michuano ya kuwania Kombe la Uhai
inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi
Kuu ya Vodacom baada ya kuifunga Tanzania Prisons mabao 2-1.
Mechi
hiyo ya kundi A imechezwa leo asubuhi (Desemba 11 mwaka huu) Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Coastal Union ilimaliza kipindi cha
kwanza ikiwa tayari imepachika mabao hayo yaliyofungwa dakika ya 24 na
33 kupitia kwa Ramadhan Same na Yusuf Chuma.
Tanzania
Prisons ambayo itacheza mechi yake pili kesho jioni (Desemba 12 mwaka
huu) Uwanja wa Azam ulioko Chamazi dhidi ya JKT Ruvu ilipata bao lake
dakika moja kabla ya filimbi ya mwisho.
Mechi
nyingine za kesho ni Toto Africans dhidi ya Coastal Union itakayochezwa
saa 2 asubuhi Uwanja wa Azam. Katika kundi B, Simba na African Lyon
zitaoneshana kazi asubuhi Uwanja wa Karume wakati Azam na Polisi
Morogoro zitacheza saa 10 jioni kwenye uwanja huo huo.
Kundi
C kesho ni Kagera Sugar vs Oljoro JKT saa 2 asubuhi Uwanja wa Karume,
na Yanga na Ruvu Shooting zitaumana saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Azam.
No comments:
Post a Comment