Tuesday, October 30, 2012

TAZAMA MATUKIO YA UTATA YA MWAMUZI MARK CLATTENBURG


Malalamiko ya Chelsea dhidi ya Mwamuzi Mark Clattenburg si yamara ya kwanza kwa refa huyu ambaye amekuwa na historia ya maamuzi yenye utata.

Mark Clattenburg, ambaye pamoja na kulalalmikiwa juu ya maauzi yake yaliyoinufaisha Man United katika mechi ya ligi kuu ya England siku ya jumapili, pia anatuhumiwa kumtolea lugha za kibaguzi mchezaji Mikel Obi

Pamoja na kuwa ni mmoja wa waamuzi wanaotambulika na FIFA na amekuwa akichezesha mechi nyingi za kimataifa lakini Clattenburg, 37, amekuwa ni mtu ambaye maisha yake ya uamuzi yamekuwa yakiandamwa na matukio ya utata.
 
AKATAA BAO HALALI LA PEDRO MENDES PALE OLD TRAFFORD  Clattenburg alifanya moja kati ya makosa makubwa katika soka wakati aliposhindwa kuliona bao la Pedro Mendes wa Tottenham Hotspurs lililovuka kwa hatua zaidi ya mbili ndani ya mstari wa lango la Manchester United.

Kipa wa Manchester United, Roy Carroll alionekana katika picha za marudio akiuokoa mpira uliotinga nyavuni. Tukio hilo liliwakera mashabiki wengi wa soka kwa sababu mpira ulikuwa umevuka kwa hatua nyingi. 
 


MSHABIKI WA NEWCASTLE ASIYECHEZESHA MECHI ZA TIMU HIYO
Clattenburg ambaye alichaguliwa rasmi kuwa mwamuzi wa Fifa mwaka 2006, akiwa na umri wa miaka 30 ni shabiki mkubwa wa Newcastle United na kutokana na hali hiyo huwa hachezeshi mechi zozote zile za kimashindano za Newcastle.

Mei 11, 2006 kutokana na mapenzi yake kwa Newcastle alichezesha pambano la kumuaga staa wa zamani wa timu hiyo, Alan Shearer lililopigwa Mei 11, 2006.



KADI NYEKUNDU YA TONY HIBBERT KWA USHAURI WA STEVEN GERRARD


 
Mwaka 2007 alijiingiza katika utata mkubwa wakati wa Merseyside derby, Liverpool na Everton. Clattenburg alionekana kusikiliza ushauri wa nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard wa kumpa kadi mlinzi wa Everton, Tony Hibbert.

Clattenburg alionekana wazi kwamba ushauri wa Gerrard ndio ulikuwa chanzo cha kumpa kadi nyekundu mlinzi huyo. Hata hivyo, baadaye Clattenburg alishindwa kumpa kadi nyekundu Dirk Kuyt kufuatia rafu mbaya aliyocheza kwa Joleon Lescott. Clattenburg hakuchezesha tena mechi yoyote ile ya Everton kwa kipindi cha miaka mitano. 





BAO LA UTATA LA LUIS NANI DHDI YA TOTTENHAM
Katika Uwanja wa Old Trafford tena mwaka 2010, na katika pambano dhidi ya Tottenham Hotspurs tena, Clattenburg aliruhusu bao lililofungwa na Luis Nani wa Manchester United kutokana na kosa la kizembe la Heurelho Gomes. Bao hilo liliwashangaza wengi na haikuonekana kama Clattenburg angeliruhusu.
  



KADI NYEKUNDU KWA CRAIG BELLAMY
Inaaminika kwenye mechi kati ya Bolton na Manchester City mwaka 2009, Clattenburg aliwauliza watu wa benchi la ufundi la City, "Mnafanya kazi vipi na Bellamy kwa wiki nzima?"

Kama ilivyo kawaida yake ya ukorofi, Bellamy alifanya vurugu zake za kawaida na Clattenburg akamtoa nje kwa kadi ya pili ya njano katika pambano hilo lililojaaa utata mwingi. Kwa mujibu wa mashuhuda, Clattenburg aliwafuata watu wa Man City na kuwauliza kwa kejeli Hivi huwa mnaishi vipi na Bellamy?


SOURCE: SHAFFIH DAUDA

No comments: