Jerry Tegete kulia na Haruna Niyonzima kushoto wakimpongeza Chuji- nyuma nyuma ni Bahanuzi 'Spider Man' |
Benchi Yanga likiomba dua wakati Chuji anakwenda kupiga penalti ya mwisho |
Said Bahanuzi 'Spider Man'' |
Mmanga akiwa kwenye machela baada ya kupoteza fahamu |
Hapa ni mara tu baada ya kuanguka akisaidiwa kwa kupepewa na wenzake |
YANGA imefuzu kuingia Nusu
Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, baada
ya kuifunga Mafunzo ya Zanzibar kwa penalti 5-4, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya
dakika 90 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wawakilishi wa Zanzibar
Mafunzo walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Ali Othman Mmanga, dakika
ya 34, akiunganisha kona ya Juma Othman Mmanga na Yanga wakasawazisha dakika ya
46, mfungaji Said Bahanuzi ‘Spider Man’.
Yanga sasa itamenyana na APR
ya Rwanda, keshokutwa ambayo katika Robo Fainali ya kwanza, imeitoa URA ya
Uganda kwa kuifunga 2-1, mabao yake yakifungwa na Jean Claude Iranzi dakika ya
tisa na Suleiman Ndikumana dakika ya 34, wakati la Watoza Ushuru wa Kampala,
lilifungwa na Robert Ssentongo dakika ya 57.
Katika mchezo huo, Juma Othman
Mmanga alipoteza fahamu na kuwaweka roho juu wachezaji wenzake na mashabiki,
akatolewa nje akipepewa na hakuweza kuendelea na mchezo, lakini taarifa za baada
ya mchezo zilisema anaendelea vizuri.
Kipa wa Yanga Berko aliumia
dakika ya 69 na akatibiwa kwa dakika tatu, kabla ya kutolewa nje dakika ya 72,
nafasi yake ikichukuliwa na Ally Mustafa Barthez ambaye ukaaji wake mazuri
langoni wakati wa penalti ulimfanya Said Mussa Shaaban wa Mafunzo akapiga nje na
kuipa Yanga ushindi.
Saidi Bahanuzi alipiga penalti
ya kwanza, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ya pili, Hamisi Kiiza ya tatu, ya
nne Haruna Niyonzima na Athumani Iddi ‘Chuji’ alipiga ya mwisho na kuwainua
maelfu ya mashabiki wa Yanga Uwanja wa Taifa.
Yanga SC; Yaw
Berko/Ally Mustafa, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin
Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Stefano Mwasyika/Idrissa Assenga, Haruna
Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Rashid Gumbo/Jerry
Tegete.
Mafunzo; Khalid Mahadhi
Hajji, Ismail Khamis Amour/Hajji Abdi Hassan, Said Mussa Shaaban, Salum Said
Shebe, Ali Othman Mmanga, Juma Othman Mmanga/Sadik Habib Rajab, Suleiman Kassim
‘Selembe’, Jaku Juma Jaku, Mohamed Abdulrahim, Wahid Ibrahim/Kheir Salum Kheir
na Ally Juma Hassan.
NI YANGA NA APR TENA NUSU FAINALI
MAHADHI MPYA; Kipa wa Mafunzo, Halid Mahadhi Haji akidaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi |
Yanga |
Mafunzo |
YANGA
imefuzu kuingia Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati,
Kombe la Kagame, baada ya kuifunga Mafunzo ya Zanzibar kwa penalti 5-4, kufuatia
sare bya 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wawakilishi wa
Zanzibar Mafunzo walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Ali Othman
Mmanga, dakika ya 34, akiunganisha kona ya Juma Othman Mmanga na Yangab
wakasawazisha dakika ya 46, mfungaji Said Bahanuzi ‘Spider Man’.
Yanga sasa itamenyana na APR
ya Rwanda, keshokutwa ambayo katika Robo Fainali ya kwanza, imeitoa URA ya
Uganda kwa kuifunga 2-1, mabao yake yakifungwa na Jean Claude Iranzi dakika ya
tisa na Suleiman Ndikumana dakika ya 34, wakati la Watoza Ushuru wa Kampala,
lilifungwa na Robert Ssentongo dakika ya 57.
Yanga SC; Yaw Berko, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Stefano Mwasyika, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Rashid Gumbo.
Yanga SC; Yaw Berko, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Stefano Mwasyika, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Rashid Gumbo.
Benchi;
Ally Mustafa ‘Barthez’, Shamte Ally, Ladislaus Mbogo, Godfrey Taita, Juma
Seif ‘Kijiko’, Jerry Tegete na Idrisa Rashid.
Mafunzo; Khalid
Mahadhi Hajji, Ismail Khamis Amour, Said Mussa Shaaban, Salum Said Shebe, Ali
Othman Mmanga, Juma Othman Mmanga, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Jaku Juma Jaku,
Mohamed Abdulrahim, Wahid Ibrahim na Ally Juma Hassan.
Benchi; Salum
Mohamed Pangani, Hajji Abdi Hassan, Kheir Salum Kheir, Sadik Habib Rajab na
Thabit Mohamed Abdallah.
MECHI YA
KWANZA....
Wachezaji wa APR wakimpongeza Ndikumana, aliyeinua vidole juu kushoto kwa kufunga bao la pili |
Dan Wagaluka wa URA kushoto akitafuta mbinu za kumtoka beki wa APR kulia |
MILIONEA WA KIARABU AWAPA SIMBA UZI MKALI WA BEI MBAYA
Wachezaji wa Simba muda si mrefu wataanza kung'aa na uzi mpya wa maana pigo za Man City |
Na Princess
Asia
KLABU ya soka ya Simba jana
imepokea msaada wa jezi, raba, viatu vya kuchezea mpira, mabegi na suti za
michezo (tracksuit) – vyote vya kisasa kabisa, kutoka kwa familia ya Al Ruwahi.
Msaada huo umetolewa kwa mapenzi mema ambayo familia hiyo inayo kwa
klabu.
Amesema
takribani miaka 30 iliyopita, familia hiihii ilitoa zawadi ya basi (Nissan
Coaster) kwa Simba na kuifanya klabu yetu kuwa ya kwanza nchini kumiliki basi
lake yenyewe.
Amesema
klabu ya soka ya Simba inatumia nafasi hii kuwakaribisha wapenzi na wanachama
wake kujitokeza kuisaidia klabu kwa namna yoyote ile, kama ilivyofanya familia
hii ya Al Ruwahi, ili kusukuma mbele gurudumu la
maendeleo
ya klabu.
"Simba
ni ya kila mmoja na haina mwenyewe. Umoja na mshikamano baina ya viongozi,
wadhamini, wapenzi na wanachama wake, ndiyo utakaoifanya izidi kuwa bora hapa
nchini na nje ya mipaka ya taifa letu,"alisema Kamwaga maarufu kama Mr.
Liverpool.
Amesema
kwa mujibu wa kanuni za mashindano haya, wachezaji wote waliokuwa na kadi moja
ya njano kwenye hatua ya makundi wamefutiwa kadi zao na hivyo Simba itaingia
uwanjani kesho Jumanne kwenye pambano dhidi ya Azam ikiwa haina mchezaji mwenye
adhabu.
Simba
imesifiwa na CECAFA kuwa ni miongoni mwa timu zenye nidhamu nzuri kwenye
michuano ya Kagame mwaka huu, mfano ukitolewa kwenye pambano lake dhidi ya AS
VITA ya DR Congo, ambapo hakukuwapo na kadi yoyote iliyotolewa mechi
nzima.
No comments:
Post a Comment