Tetesi za J'tatu magazeti ya Ulaya
HATIMAYE MAN UNITED YAMNASA LUCAS MOURA KWA PAUNI MILIONI 26
KLABU ya Manchester United
imekubali kutoa dau la pauni Milioni 26 kuinunua saini ya kinda Mbrazil, Lucas
Moura, mwenye umri wa miaka 19, kutoka Sao Paulo.
MAN
United pia iko tayari kumsajili nyota wa Fulham, Moussa Dembele, mwenye umri wa
miaka 25.
KLABU
ya Arsenal inataka mshambuliaji wake anayetaka kuhama, Robin van Persie adai
pauni Milioni 10.1 kwa mwaka, iwe Manchester United, City au Juventus ambazo
zote zinamtaka Mholanzi huyo.
KLABU
ya Manchester City imetega mitego yake kwa Daniele De Rossi, mwenye umri wa
miaka 28, kwa mara nyingine tena baada ya kushindwa kumpata Mtaliano huyo msimu
uliopita.
KLABU
ya Tottenham anamtaka mshambuliaji wa AS Roma, Marco Borriello, mwenye umri wa
miaka 30, baada ya kuambiwa hawana nafasi ya kumsajili nyota wa Atletico Madrid,
Adrian Lopez.
MCHEZAJI
mwenye mkataba na Blackburn Rovers, Junior Hoilett hatajiunga na Queens Park
Rangers, vinginevyo klabu hiyo ya London ilipe dau la pauni Milioni 6 au
pendekezo la kubadilishana na Jamie Mackie.
KLABU
mpya katika Ligi Kuu ya England, Southampton inataka kumsajili beki wa
Blackburn, Scott Dann, mwenye umri wa miaka 25.
KLABU
ya Fulham imempata kwa mkopo wa muda mrefu mshambuliaji wa Chelsea mwenye
thamani ya pauni Milioni 18, Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 19.
KLABU
ya Crystal Palace inaweza kuendelea kuboresha kikosi chake kwa kumsajili
mshambuliaji wa KIfaransa, Alexis Allart,mwenye umri wa miaka 25, ambaye
atawagharimu pauni 300,000
AVB AKERWA NA MODRIC
KOCHA
wa Tottenham, Andre Villas-Boas amekerwa na kitendo cha kiungo anayetaka kuhama
klabu hiyo, Luka Modric raia wa Croatia kutoonekana mazoezini .
MWENYEKITI
mwenye hasira kali nwa Spurs, Daniel Levy anaweza kuzuia uhamisho wowote wa Luca
Modric baada ya mchezaji hujyo kutoonekana mazoezini mwishoni mwa wiki na
atamtoza faini mchezaji huyo kwa mara ya tatu ndani ya siku nne ikiwa atashindwa
kuhudhuria mazoezi na leo.
BALOTELLI ANAKUFURU JAMANI..
MSHAMBULIAJI
wa Manchester City, Mario Balotelli, mwenye umri wa miaka 21, amevunja rekodi ya
matumizi kwa jinsi anavyotumia katika holiday yake huko Ibiza na kulipa 'bill'
kubwa kubwa.
YANGA WASAKA NUSU FAINALI LEO
Kikosi cha Yanga kilichoipiga APR 2-0 |
Na Prince
Akbar
MABINGWA watetezi wa Klabu
Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Yanga SC ya Dar es
Salaam, leo wanashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kumenyana
na Mafunzo ya Zanzibar katika hatua ya Robo Fainali ya michuano
hiyo.
Kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom
Saintfiet katika mchezo wa leo, atamkosa kiungo Nizar Khalfan ambaye
anasumbuliwa na maradhi ya nyonga, wakati hali ya kinara wa mabao wa timu hiyo,
Said Bahanuzi ‘Spider Man’ hadi jana haikuwa ya kumpa uhakika wa kucheza mechi
hiyo.
Bahanuzi anasumbuliwa na
maumivu ya mgongo, wakat kiungo Nizar Khalfan yeye kwa asilimia 100 hatacheza
kutokana na maumivu hayo ya nyonga.
Saintfiet aliiambia BIN
ZUBEIRY jana kwamba, Nizar hatacheza kabisa, lakini wachezaji wengine
watatu, Bahanuzi, kipa Yaw Berko anayesumbuliwa na goti, kiungo Athumani Iddi
‘Chuji’ na Hamisi Kiiza wanaosumbuliwa na quadriceps wako kwenye hatihati
kucheza.
Mtakatifu Tom amesema kwamba,
Daktari wa Yanga, Sufiani Juma anaendelea kufuatilia kwa karibu hali za
Bahanuzi, Kiiza, Berko na Chuji ili kuhakikisha wanakuwa fiti kwa ajili ya mechi
ya leo.
Amesema sababu ya wachezaji
wake kuumia mara kwa mara ni kutokana na kucheza mechi mfululizo na kulingana na
kanuni za mashindano hayo, hawezi kutumia wachezaji zaidi ya 20, hivyo hana
namna nyingine zaidi ya kupambana na hali hiyo.
Bahanuzi ndiye kinara wa mabao
wa Yanga hivi sasa, hadi sasa akiwa amekwishaifungia timu hiyo mabao manne,
hivyo kuingia kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha mashindano hayo,
ambayo tayari kwenye kabati la Yanga kuna mataji manne
yamehifadhiwa.
Mshambuliaji huyo mpya kutoka
Mtibwa Sugar ya Morogoro, Ijumaa alikaribia kuondoka na mpira uwanjani, kama si
refa Dennis Batte kutoka Uganda kukataa bao lake moja siku ambayo alifunga
mawili yaliyokubaliwa dhidi ya APR ya Rwanda, Yanga ikishinda 2-0, Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
Katika mchezo huo, Kocha Tom
alimpumzisha Bahanuzi dakika ya 72 na nafasi yake ikachukuliwa na Jerry Tegete,
wakati Nizar Khalfan kabla ya hapo alimpisha Juma Seif ‘Kijiko’.
Matatizo ya
mgongo kwa Spider Man yalianzia kwenye mechi na APR |
Mchezo kati ya Yanga na
Mafunzo, utaanza saa 10:00 jioni na utatanguliwa na mechi nyingine ya Robo
Fainali kati ya URA ya Uganda na APR ya Rwanda, wakati kesho Atletico Olympique
Sport ya Burundi itamenyana na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
katika Robo ya Fainali ya tatu mchana, kabla ya Azam FC na Simba SC, zote za Dar
es Salaam, kuhitimisha awamu ya Nane Bora ya michuano hiyo.
Michuano hii, iliyoanza Julai
14 na inatarajiwa kufikia tamati Julai 28, inadhaminiwa na Azam na SuperSport
Televisheni.
RATIBA ROBO
FAINALI
Julai 23, 2012
URA
vs APR (Saa 8:00 mchana)
Mafunzo vs Yanga (Saa
10:00 jioni)
Julai 24,
July
Atletico vs AS Vita (Saa
8:00 mchana)
Azam vs Simba SC (Saa
10:000 jioni)
WIKI MBILI KUAMUA HATIMA YA OKWI BUNDESLIGA
Okwi |
Na Princess
Asia
EMMANUEL Okwi, mshambuliaji wa
Simba SC amepewa wiki mbili zaidi za kuendelea na majaribio katika klabu ya FC
Red Bull Salzburg ya Austria yenye maskani yake Wals-Siezenheim, nchini humo na
baada ya hapo ndipo majibu yatatoka.
Katibu wa Simba Evodius
Mtawala ameiambia BIN ZUBEIRY jana usiku kwamba, Okwi ambaye
tayari yuko huko kwa wiki moja, hadi sasa anafanya vizuri ndio maana kapewa wiki
mbili zaidi, ili kocha wa klabu hiyo ajiridhishe zaidi na kiwango cha Mganda
huyo.
Klabu hiyo inayotumia Uwanja
wa Red Bull Arena, ikiwa zaidi inafahamika kama SV Austria Salzburg kabla
haijanunuliwa na kampuni ya Red Bull mwaka 2005, imewahi kufika Fainali ya Kombe
la UEFA mwaka 1994 na inacheza Ligi Kuu ya Austria, iitwayo Bundesliga kama Ligi
Kuu ya Ujerumani.
Timu hiyo ni kama timu ambayo
Okwi, anachezea kwa sasa, Simba SC, kwani nayo inavaa jezi za rangi ya nyeupe na
nyekundu na imewahi kutwaa taji la Bundesliga ya Austria mara saba na pia
ilicheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 1994–1995 kama Casino Salzburg, na kuwa
timu pekee, ambayo haikufungwa na mabingwa wa wakati huo, Ajax
Amsterdam.
Awali, Okwi aliikosesha Simba
Sh. Bilioni 2 kwa kukataa kujiunga na klabu ya Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini
na kuamua kwenda Austria, ambako inaelezwa klabu hiyo iko tayari kutoa Euro
600,000 akifuzu.
Awali Olando Pirates ya Afrika
Kusini ilimuomba Okwi akafanye majaribio huko kama angefuzu wangemsajili dau la
dola 550,000 kabla ya kuibuka kwa taarifa za kutakiwa Italia na klabu ya
Parma.
Hata hivyo, Simba SC ilisema
imeshindwa kumshawishi Okwi kwenda kucheza Afrika Kusini kwa kuwa mwenyewe
anataka kucheza Ulaya tu. Wakala aliyeiunganisha Simba na Pirates akawasilisha
ofa nyingine kutoka Mamelodi, ambayo ni Euro 600,000 na kupanda hadi Sh. Bilioni
2, lakini bado mabingwa hao wa Tanzania, walishindwa kumshawishi Okwi kwenda
Ligi Kuu ya Afika Kusini (PSL).
MANJI NA JESHI LAKE LA MIAMVULI WAWAPA SUMU WACHEZAJI YANGA KUUA WAZENJI KESHO
Wapiganaji wa Yanga wakiteta kabla ya
kuzungumza na wachezaji leo
Makamu Mwenyekiti wa Yanga,
Clement Sanga akiwaeleza jambo viongozi wenzake wa
Yanga
Manji, Sanga, Katabalo na Bin
Kleb wakijadiliana jambo kabla ya kuzungumza na
wachezaji
Manji akiondoka klabuni kwa
gari lake binafsi baada ya kuzungumza na wachezaji leo. (Picha zote na Emmanuel
Ndege wa blogu ya Liwazozito).
MWENYEKITI wa klabu ya Yanga,
Yussuf Manji leo ametembelea tena makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na
Jangwani, Dar es Salaam na kuzungumza na wachezaji.
Manji alifika klabuni hapo
akiwa ameongozana na makamu wake, Clement Sanga, wajumbe wa kamati ya utendaji,
Abdalla Bin Kleb na Mussa Katabalo pamoja na aliyekuwa makamu mwenyekiti wa
kamati ya usajili, Seif Ahmed.
Viongozi hao walikutana na
wachezaji kwa saa kadhaa na kuzungumza nao mambo mbalimbali kwa lengo la
kuwaweka sawa kabla ya mechi yao ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Kagame
dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar.
Yanga inatarajiwa kushuka
dimbani leo kucheza na Mafunzo katika mechi ya pili ya robo fainali itakayoanza
saa 10 jioni. Katika mechi ya awali, URA ya Uganda itavaana na APR ya
Rwanda.
Katika kikao hicho cha
faragha, inasemekana kuwa Manji na viongozi wenzake waliwataka wachezaji
kutambua vyema jukumu lililo mbele yao na kuongeza jitihada ili waweze kufika
mbali zaidi.
Alisema mechi hiyo ni muhimu
kwao kwa vile iwapo wataishinda Mafunzo watafuzu kucheza nusu fainali na hivyo
kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutwaa
ubingwa.
SAMATTA ATOA PASI MBILI ZA MABAO, MAZEMBE IKIBANWA 2-2 NA CHELSEA NYUMBANI
Samatta. Picha ta Maktaba |
Mshambuliaji chipukizi wa
kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ‘Sama Goal’, leo ametoa pasi zote za
mabao mawili ya klabu yake, Tout Puissant Mazembe, kwenye Uwanja wa TP Mazembe
mjini Lubumbashi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Berekum
Chelsea ya Ghana, uliomalizika hivi punde kwa sare ya 2-2.
Mapande yote ya Samatta leo
yalitumiwa vema na Tressor Mputu Mabi katika dakika za 11 na 32 kuipatia mabao
Mazembe, wakati Chelsea ya Ghana ilionyesha yenyewe ni moto kweli kwa kupata
sare Lubumbashi. Mabao ya Chelsea yalifungwa na Emmanuel Atukwei Clottey katika
dakika za 71 na 84. Dakika ya 75, Samatta alimpisha Francis Kasonde wakati huo
wenyeji wakiwa wanangoza 2-1, lakini kutoka kwake kulisababisha jahazi kuzama
kabisa.
Katika mchezo wa kwanza,
Mazembe ilifungwa 1-0 wiki iliyopita, Samatta akifunga bao la kufutia machozi
Cairo na sasa mabingwa hao mara nne Afrika wana pointi moja tu ndani ya mechi
mbili, kuashiria kwamba wana kibarua kizito kutimiza ndoto zao za kutwaa ndoo ya
tano Afrika.
Mechi nyingine ya Kundi lao,
itafuatia saa 5:00 usiku, kati ya wapinzani wa jadi katika soka ya Misri,
Zamalek na Al Ahly.
SPIDER MAN HATARINI KUWAKOSA MAFUNZO, NIZAR HATA JEZI HAVAI KESHO, BERKO, CHUJI, KIIZA NAO NJE NDANI
Said Bahanuzi 'Spider Man' |
Na Prince
Akbar
MSHAMBULIAJI tegemeo wa Yanga,
Said Bahanuzi ‘Spider Man’ yuko hatarini kuikosa mechi ya Robo Fainali ya Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kesho dhidi ya Mafunzo ya
Zanzibar, kutokana na maumivu ya mgongo, wakat kiungo Nizar Khalfan yeye kwa
asilimia 100 hatacheza kutokana na maumivu ya nyonga.
Kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom
Saintfiet ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba, Nizar hatacheza
kabisa, lakini wachezaji wengine watatu, Bahanuzi, kipa Yaw Berko
anayesumbuliwa na goti, kiungo Athumani Iddi ‘Chuji’ na Hamisi Kiiza
wanaosumbuliwa na quadriceps wako kwenye hatihati kucheza.
Mtakatifu Tom amesema kwamba,
Daktari wa Yanga, Sufiani Juma anaendelea kufuatilia afya za Bahanuzi, Kiiza,
Berko na Chuji ili kuhakikisha wanakuwa fiti kwa ajili ya mechi ya kesho, lakini
kwa Nizar kocha huyo wa zamani wa Namibia na Ethiopia, amekwishakata tamaa
kumtumia kwenye mechi na Mafunzo.
Amesema sababu ya wachezaji
wake kuumia mara kwa mara ni kutokana na kucheza mechi mfululizo na kulingana na
kanuni za mashindano hayo, hawezi kutumia wachezaji zaidi ya 20, hivyo hana
namna nyingine zaidi ya kupambana na hali hiyo.
Bahanuzi ndiye kinara wa mabao
wa Yanga hivi sasa, hadi sasa akiwa amekwishaifungia timu hiyo mabao manne,
hivyo kuingia kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha mashindano hayo,
ambayo tayari kwenye kabati la Yanga kuna mataji manne
yamehifadhiwa.
Mshambuliaji huyo mpya kutoka
Mtibwa Sugar ya Morogoro, juzi alikaribia kuondoka na mpira uwanjani, kama si
refa Dennis Batte kutoka Uganda kukataa bao lake moja siku ambayo alifunga
mawili yaliyokubaliwa dhidi ya APR ya Rwanda, Yanga ikishinda 2-0, Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
Katika mchezo huo, Kocha Tom
alimpumzisha Bahanuzi dakika ya 72 na nafasi yake ikachukuliwa na Jerry Tegete,
wakati Nizar Khalfan kabla ya hapo alimpisha Juma Seif ‘Kijiko’.
Wakati huo huo: Baraza la
Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), leo limesema kwamba mechi ya
Yanga kesho itakuwa ya pili, kama ambavyo itakuwa kwa Simba
keshokutwa.
RATIBA ROBO
FAINALI
Julai 23, 2012
URA
vs APR (Saa 8:00 mchana)
Mafunzo vs Yanga (Saa
10:00 jioni)
Julai 24,
July
Atletico vs AS Vita (Saa
8:00 mchana)
Azam vs Simba SC (Saa
10:000 jioni)
No comments:
Post a Comment