Thursday, June 21, 2012
KENNETH ASAMOAH ATEMWA YANGA - KULIPWA FIDIA
Hatimaye mshambuliaji
wa Yanga kutoka Ghana Kenneth Asamoah ametemwa na klabu hiyo baada ya kuitumikia
kwa takribani msimu mmoja tu.
Kwa mujibu wa taarifa
kutoka ndani ya Yanga, Asamoah amefikia makubaliano na Yanga kwa kulipwa fidia
ya kuvunjiwa mkataba wake aliousaini msimu uliopita.
Kenneth Asamoah
anaondoka Yanga huku akiwaachia wapenzi wa klabu hiyo kumbukumbu ya goli zuri la
kichwa alilowafunga Simba kwenye fainali ya kombe la Kagame mwaka jana kwenye
uwanja wa Taifa.
SIKU KAMA YA LEO: WAYNE ROONEY AFUNGA GOLI LAKE LA KWANZA KWENYE EURO - SPAIN WABEBA UBINGWA WAKWANZA ULAYA 1964
Baada ya kupoteza ushindi dakika za mwisho kwenye
mchezo wao ufunguzi wa Euro 2004 kwa Ufaransa, England wakaanza kampeni yao
vizuri kwenye mechi ya pili kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya
Switzerland.
Kijana wa miaka 18Wayne Rooney alifunga mara mbili akijitangaza kwenye ulimwengu wa soka, huku Steven Gerrard akifunga goli la tatu.
England na Rooney waliendeleza mazuri waliyoyafanya siku kama hii, walipokutana na Croatia kwenye mechi ya mwisho ya group. Lakini hayakuanza vizuri kwa vijana wa Sven Goran Eriksson baada ya Niko Kovac kufungagoli la kuongoza kwa Croatia.
Three lions walihangaika mpaka pale kwenye dakika ya 40, Paul Scholes aliposawazisha - goli la mwisho alilofunga kwa ajili ya nchi yake.
Wayne Rooney baadae kafunga bao la pili kabla ya timu mbili kwenda mapumziko. Baadae Frank Lampard akafunga bao la nne.
Ushindi huo ulimaanisha England wameshinda mechi mbili mfululizo za Euro, ikiwa ni mara ya pili kufanya hivyo, baada ya kuwafunga Scotland na Holland mwaka 1996.
Ushindi huo pia uliweka rekodi nyingie baada ya England kuingia robo fainali kwa mara ya kwanza kwenye historia ya michuano hiyo wakati Euro inapofanyika nje ya ardhi ya England.
Pia siku kama ya leo Spain waliifunga Soviet Union na kufanikiwa kushinda kombe la Euro 1964

TETESI HAI - NYUMBANI NI NYUMBANI: MRISHO NGASSA NJIANI KURUDI YANGA
Yanga wameendelea
kuonyesha mabavu katika usajili baada ya kumsajili Kelvin Yondani, Nizar
Khalfan, Barthez, Domayo na wengine wengi, leo taarifa za usajili kutoka klabu
hiyo zinasema kwamba klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Azam ili
kuweza kumsajili winga wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Khalfan
Ngassa.
Habari za ndani
zinadai kwamba zinadai kwamba Ngassa, Yanga na Azam wapo kwenye mazungumzo ya
mwisho na huenda kesho kutakuwa na habari nzuri kwa wapenzi wa Yanga juu ya
kurudi kwa kipenzi chao Ngassa mitaa ya Jangwani.
"Leo saa nne asubuhi Ngassa alifika pale makao makuu ya Yanga na akawa kwenye kikao kizito katibu wa Yanga na mmoja wa wadau wakubwa wa Yanga bwana Seif." - kilisema chanzo cha habari.
"Leo saa nne asubuhi Ngassa alifika pale makao makuu ya Yanga na akawa kwenye kikao kizito katibu wa Yanga na mmoja wa wadau wakubwa wa Yanga bwana Seif." - kilisema chanzo cha habari.
Katika usajili huo
Yanga wapo tayari kulipa kiasi kikubwa cha fedha na kumtoa kiungo Nurdin Bakary
ili kuweza kumtwaa winga huyo ambaye alishwahi kuichezea Yanga kwa mafanikio
kalba ya kuhama kwa uhamisho uliovunja rekodi ya ndani ya usajili baada ya Azam
kulipa milioni 60 kwa Yanga na kumtwaa Ngassa
No comments:
Post a Comment