Hatimae wekundu wa msimbazi Simba leo hii wamefanikiwa
kumsajili beki MASOMBO LINO kutoka klabu ya Dc Motema Pembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
Masombo Lino amabaye anacheza nafasi ya beki wa kati amekamilisha uhamisho mara tu baada ya kutua nchini leo asubuhi, awali Simba ilitaka kumsajili beki wa zamani wa Étoile Sportive du Sahel ya nchini Tunisia Gladys Bokese amabaye kwasasa anaichezea Dc Motema Pembe lakini imesitisha mpango huo na kuamua kumpa kibarua MASOMBO.

OKWI AGEUKA LULU SOKO LA USAJILI: SASA TIMU MOJA YA SERIE A NA MAMELODI SUNDOWNS ZAGOMBEA SAINI YAKE
Nyota ya mshambuliaji wa
kimataifa wa Simba raia wa Uganda Emmanuel Okwi, inazidi kuwaka, siku chache
baada ya klabu bingwa ya Orlando Pirates kutuma barua ya kumtaka mshambuliaji
huyo wa Simba aende kufanya majaribio kwenye klabu hiyo, leo hii timu pinzani ya
Orlando kwenye ligi ya Afrika kusini, Mamelodi Sundowns wameuambia uongozi wa
Simba kwamba wapo tayari kumnunua mshambuliaji huyo.
Taarifa zilizothibitishwa
kutoka ndani ya uongozi wa Simba zinasema kwamba Mamelodi wametuma maombi ya
kutaka kumsaini Okwi ambaye amekuwa na msimu mzuri sana ndani na nje ya ligi kuu
ya Vodacom msimu ulioisha.
Pia chanzo changu hicho
cha habari kutoka ndani ya Simba kilisema kwamba kuna timu moja inayoshiriki
ligi kuu ya Italia Serie A, wameonyesha nia ya kumtaka Okwi lakini wamesema
kwamba wanasubiri mpaka michuano ya Euro itakapoisha ndipo watakapoamua juu ya
suala la usajili wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda
No comments:
Post a Comment