Friday, October 28, 2016

Wakulima wa Nanyumbu kuuza korosho zao hadi sh. 3,800

Meneja mkuu wa Chama kikuu cha ushirika cha Masasi, Mtwara C operative Union- MAMCU Kelvin Rajab akitoa maelekezo kwa wakulima wa korosho wa Nanyumbu katika mada ulioendeshwa na chama hicho katika ghala la Mangaka AMCOS.

Baadhi ya wakulima wa korosho wa wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara wakiwa katika mnada wa ununuzi wa zao hilo katika Ghala la chama cha msingi cha Mangaka. Mnada umeendeshwa na chama kikuu cha ushirika cha Masasi, Mtwara Co operative Union- MAMCU

 

Baadhi ya wakulima wa korosho wa wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara wakiwa katika mnada wa ununuzi wa zao hilo katika Ghala la chama cha msingi cha Mangaka. Mnada umeendeshwa na chama kikuu cha ushirika cha Masasi, Mtwara Co operative Union- MAMCU. Pia wapo viongozi wa bodi ya korosho.




Kelvin Rajab




Meneja mkuu wa Chama kikuu cha ushirika cha Masasi, Mtwara C operative Union- MAMCU Kelvin Rajab akifungua sanduku la barua za kuomba tenda ya ununuzi wa korosho za wakulima wa Nanyumbu katika mada ulioendeshwa na chama hicho katika ghala la Mangaka AMCOS.

Mnada wa Tatu wa chama kikuu cha ushirika cha Masasi, Mtwara Co operative Union- MAMCU umemalizika hapa katika ghala la chama cha msingi cha Mangaka, kwa kushuhudia wakulima wa wilaya ya Nanyumbu wakitarajia kuuza korosho zao kwa bei ya juu ya sh. 3,800 na bei ya chini ya sh. 3, 788.

Kampuni za ununuzi wa zao hilo za Star Nuts na Tanzashamba zimefanikiwa kushinda kwa tenda ya ununuzi huo kwa bei ya juu ya sh. 3, 800 huku kampuni ya Machinga ikipata tenda ya ununuzi kwa bei ya sh. 3, 790 na ile ya CDGKL ikipata kwa sh. 3,788.


No comments: