Monday, July 14, 2014

SCOLARI ATIMULIWA KAZI SAA 1 BAADA YA MECHI YA FAINALI


LUIZ FELIPE SCOLARI

Na Juma Mohamed

Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) limemtimua kocha wa timu ya taifa Luiz Felipe Scolari  saa chache baada ya kumalizika kwa mechi ya fainali pale Ujerumani ilipoilaza Argentina na kushinda Kombe la Dunia.
Scolari alisema angeacha CBF waamue hatima yake baada ya timu yake kushindwa 3-0 na Uholanzi mechi ya kuamua wa kumaliza nambari tatu Jumamosi, na baada ya kuaibishwa 7-1 na Ujerumani Jumanne.
Uchezaji huo wa Jumanne ulikuwa mbaya zaidi kwa taifa hilo tangu kushindwa fainali ya 1950 na Uruguay michuano  ilililoandaliwa Brazil, kovu katika historia ya soka ya taifa hilo na ambalo huitwa Maracanazo kutokana na uwanja wa Maracana kulikochezewa fainali hiyo.
Scolari, anayejulikana sana kwa lakabu yake ya Felipao, aliongoza Brazil kushinda Kombe la Dunia 2002 nchini Japan. Alichukua tena usukani Desemba 2012, kabla ya kuandaa michuano ya Kombe la Confederations.
Brazil walishinda michuano hiyo, inayochukuliwa kama kipasha moto cha Kombe la Dunia, kwa kulaza waliokuwa mabingwa wa dunia wakati huo Uhispania 3-0.
Baada ya hapo Brazil walianza kujiandaa kwa waliotarajia kuwa ushindi wao wa sita wa Kombe la Dunia nyumbani kwao.
Wakosoaji wake hata hivyo bado hawajaridhishwa na hatua ya Scolari ya kutokuwa na uchezaji maridadi na kutumia mbinu kali.

SOURCE: SUPERSPORT

1 comment:

Juma Mohamed said...

Amestaili huyu mzeee...tena wamemchelewesha, ilibidi pale baada ya zile 7