Sunday, June 17, 2012

Taifa Stars yatolewa kwa penalti

 

Taifa Stars imetolewa kwenye mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kufungwa kwa penalti na wenyeji Msumbiji (The Mambas) katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa ulioko Zimpeto pembeni kidogo ya Jiji la Maputo.

Refa Bennett Daniel alipopuliza filimbi ya kumaliza dakika 90 za pambano hilo timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, hivyo kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) mikwaju ya penalti ikatumika kupata mshindi.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam, Februari 29 mwaka huu timu hizo
zilitoka sare ya bao 1-1.

Msumbiji ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 9 lililofungwa na mshambuliaji Jeremias Sitoe akiungnisha krosi ya Elias Pelembe ambaye mabeki wa Taifa Stars walifikiri ameotea.

Stars ilisawazisha bao hilo dakika ya 89 likifungwa kwa kichwa na
Aggrey Morris kutokana na mpira wa kona uliopigwa Amir Maftah.

Mikwaju ya penalti tano tano walioifungia Stars walikuwa Amir Maftah, Shabani Nditi na Shomari Kapombe wakati Aggrey Morris na Kevin Yondani walikosa.

Kwa vile The Mambas nao walikosa mbili ikabidi iongezwe penalti moja moja. Waliofunga kwa upande wa Stars walikuwa John Bocco, Frank Domayo na Mrisho Ngassa wakati Mbwana Samata alikosa.

Akizungumzia pambano hilo, Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen aliwapongeza wachezaji wake kwa kupambana hadi dakika ya mwisho.

"Tulikuja Maputo tukijua kuwa tunatakiwa kufunga bao, tumeweza kufunga bao ingawa katika dakika za mwisho. Unajua linapokuwa suala la penalti chochote kinaweza kutokea, na ndivyo ilivyokuwa," alisema Kim.

Taifa Stars itarejea nyumbani Juni 19 mwaka huu, ambapo itaaondoka hapa saa 4.40 asubuhi kwa kupitia Nairobi, Kenya na kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 1.50 usiku.

Kikosi kilipngwa hivi; Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni/John Bocco, Aggrey Morris, Kevin Yondani, Shaabani Nditi, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Thomas Ulimwengu/Haruna Moshi, Mbwana Samata na Mwinyi Kazimoto/Amir Maftah.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MHARIRI GAZETI LA BINGWA AFARIKI DUNIA


Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (kushoto)
akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya
Waziri Mkuu Jamhuri ya Uturuki (Idara ya Habari na Maelezo),
Murat Karakaya iliyotolewa kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu
Uturuki, Bulent Arinc aliyemwakilisha Waziri Mkuu wa nchi
hiyo, Recep Tayyip Erdogan, baada ya kuwasilisha mada katika
mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki
kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita
dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki
iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu,
ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau
wengine kutoka nchi 54 za Afrika.


MHARIRI wa Jamboleo, Willy Edward Ogunde amefariki dunia mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo (saa 6.30) usiku.

Taarifa ya Neville Meena, Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, imesema kwamba Willy aliyewahi kuwa Mhariri wa gazeti la BINGWA, pamoja na wahariri wengine walikuwa mjini Morogoro ambako walikwenda kuhudhuria mkutano wa masuala ya sensa iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Mara baada ya semina hiyo alikwenda kuwaona watoto wake na alikuwa huko hadi saa sita usiku alipomwita dereva wa pikipiki afike kumchukua kwa lengo la kurejea katika hoteli alikokuwa amefikia. Baada ya kutoka nje, na hatua sita hivi kabla ya kufika pikipiki ilipokuwa, alianguka.
Ndugu zake walimkimbiza hosipitali lakini walipofika na daktari kumpima, tayari alikuwa “amenyamaza” yaani amefariki dunia. Taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Dar es Salaam zinafanywa.
Tutamkumbuka daima kwa upole na unyeyekevu wake. Kweli Willy ametuacha, ni pigo kwa taaluma yetu, ni pogo katika Jukwaa la Wahariri. Poleni kwa familia ya Willy Edward Ogunde, pole kwa wahariri wote na pole kwa tasnia nzima ya habari. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

MSUMBIJI YAIFUNGA TAIFA STARS KWA MIKWAJU YA PENALTI.

Timu ya taifa ya Msumbiji imefanikiwa kuitoa timu ya taifa ya Tanzania kwa mikwaju ya penalti kwenye kinyang'anyiro cha kusaka tiketi ya kufuzu AFCON 2012.
Mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo kufungana bao 1:1.

Habari kamili itafuata....................

HISTORIA INAWAHUKUMU UHOLANZI DHID YA URENO: AKINA VAN PERSIE HAWAJAFUNGA AKINA ONALDO NDANI YA MIAKA 10 ILIYOPITA.

Uholanzi inabidi washinde mechi yao dhidi ya Ureno kwa goli 2-0 au zaidi, na kuombea Ujerumani wawafunge Denmark ili kuweza kuendelea kwenye robo fainali, lakini historia inawahukumu wadachi dhidi ya Wareno.

Matokeo ya nyuma yanaonyesha Ureno wana nafasi kubwa kupata matokeo chanya na kuwafunga vijana wa Bert van Marwijk katika mchezo muhimu wa mwisho wa kundi B leo jumapili.

Tofauti na wanapokutana na wababe wao Wajerumani ambao wamekuwa wakionea sana Ureno katika mechi 16 za mwisho zilizowakutanisha timu hizo, Ureno wamefanikiwa kushinda mechi 3, Ureno nayo imekua ikiionea sana Uholanzi kwenye mechi zao nyingi walizokutana.

Ureno walipata matokeo dhidi ya Uholanzi katika mechi zifuatazo, wakiwafunga kwenye hatua ya 16 bora kwenye kombe la dunia 2006, kwenye nusu fainali ya Euro 2004 wakwafunga tena 2-1, na kwenye kufuzu kombe la dunia 2002 wakawatungua 2-0, na Euro 92 kwa 1-0. Pia hawajawahi kufungwa na Uholanzi kwenye mechi za kirafiki.

Mechi pekee ambayo Wadachi waliwafunga Ureno ilikuwa mwezI wa 10, 1991 mjini Rotterdam kwa 1-0 katika mechi za kufuzu Euro. Robert Witchge aliwafungia The Oranje goli pekee.

Kama wataweza kuwafunga Ureno kwa mara ya pili kwenye historia yao kwa idadi ya magoli mawili au zaidi, basi itabidi wasali na kuomba Denmark wafanye walichofanya miaka 10 iliyopita kwenye Euro 1992 kwa kuwafunga tena Ujerumani.

FERNANDO TORRES NDIO KAISHIKA BAHATI YA SPAIN: HAIJAWAHI KUFUNGWA KILA TORRES ANAPOFUNGA

Spain walipiga hatua muhimu kuelekea kwenye robo fainali ya michuano ya Euro 2012 alhamisi iliyopita kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya Jamhuri ya Ireland. Kwenye mechi yao ya kwanza dhidi ya Italia, La Roja waliacha mashaka makubwa kwenye kiwango chao ambacho kilifeli kuwashinda Waitaliano, huku Cesc Fabregas akianza katika mfumo wa kuchezesha timu bila kuwa na mshambuliaji halisi. Lakini kwenye mchezo wao wa pili, Fernando Torres akianza badala ya Fabregas, Spain walirudisha kiwango chao, wakicheza kwa kuelewana zaidi, pasi nzuri na za maana na kikubwa zaidi walipata magoli.

Kwenye mchezo wao ufunguzi, kocha Vicente De Bosque alianzisha kikosi kisichokuwa na mshambuliaji halisi na alitupia lawama nyingi baada ya mchezo, japokuwa Fabregas aliyecheza kama mshambuliaji kivuli, alifunga goli pekee la kusawazisha goli la Antonio Di Natale. Torres aliingia kama sub dakika ya 16 kabla ya mchezo wa kumalizika lakini hakuweza kubadili matokeo ya sare, pamoja na kupata nafasi mbili za wazi mwishoni mwa mchezo huo. Dhidi ya Ireland, magoli yake mawili yalionyesha ni kiasi gani ana umuhimu kwenye kikosi cha kwanza.


Torres alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi na Uefa, pia akafikia rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu kwa kuifungia Spain magoli mengi, akiwa na goli 30. Akimpita Fernando Hierro mwenye magoli 29, huku akiwa nyuma ya Raul mwenye 44, na David Villa mwenye mabao 51.

El Nino, 28, ambaye alifunga goli pekee liloipa ubingwa wa Euro 2008 Spain, wakati walipoifunga Ujerumani na kumaliza ukame wa miaka 44 wa makombe nchini Austria na Switzerland, amekuwa na bahati sna ndani ya timu ya taifa, La Roja haijawahi kupoteza mechi ambayo Fernando Torres anafunga.

Spain wameshinda mechi za 21 za mwisho ambazo Torres anakuwa amefunga. Mechi pekee ambayo Fernando alifunga na Spain wakashindwa kushinda ilikuwa mwaka 2004 mjini Genoa, dhidi Italy. Hili ndilo lilikuwa goli la kwanza la Torres kuifungia La Roja.

Katika magoli yake 30, zimekuwepo hat ticks mbili, moja dhidi ya San Marino na nyingine dhidi ya New Zealand, akifunga ndani ya dakika 17 za mchezo kwenye kombe la mabara, na kuweka rekodi ya kuwa hat tick ya haraka zaidi katika historia ya La Roja.

Italy, San Marino, China, Belgium, Slavakia, Croatia, Ukraine, Tunisia, Liechtenstein, Latvia, Sweden, Germany, Chille, Azerbaijan, New Zealand, Macedonia, Poland, United States, South Korea na sasa Ireland timu hizi zote zimekutana na balaa la Fernando Torres, huku goli muhimu zaidi likiwa lile alilowafunga vijana wa Joachim Low kwenye fainali ya Euro 2008.

So mashabiki wa Spain sasa itabidi waombe kuwepo na ufanano huu kwa mshambulaiji huyu ili kuweza kufanikisha azma yao ya kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuchukua makombe matatu makubwa mfululizo.

No comments: