KUNDI la
al-Shabab nchini Somalia limesema wapiganaji wake wameshambulia kambi ya
wanajeshi wa Kenya wanaohudumu chini ya kikosi cha Umoja wa Afrika
(Amisom)nchini Somalia.
Wapiganaji hao
wanadai kuwaua wanajeshi wengi kwenye shambulio hilo katika kambi ya Kulbiyow
kusini mwa Somalia karibu na mpaka wa nchi hiyo na Kenya.
"Mujahideen
(wapiganaji) wawili walivurumisha magari yaliyokuwa na mabomu na kuyalipua
kwenye lango la kambi hiyo ya mji wa Kulbiyow kabla ya wapiganaji wengine
kuingia. Baada ya makabiliano makali, tumefanikiwa kuiteka kambi," mmoja
wa wasemaji wa al-Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab ameambia shirika la habari
la Reuters.
Msemaji huyo
amedai kundi hilo limewaua wanajeshi zaidi ya 50 na kutwaa magari na silaha za
wanajeshi hao, taarifa ambazo msemaji wa majeshi ya Kenya amekanusha.
Kanali Paul
Njuguna ameambia Reuters: "Ni uongo. Operesheni ya kijeshi inaendelea.
Tunaendelea kupokea taarifa."
Al-Shabab
wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya inayoungwa mkono na mataifa ya
magharibi na jamii ya kimataifa.
Wanajeshi wa
Kenya pamoja na wanajeshi kutoka Djibouti, Uganda na Ethiopia, chini ya Amisom,
wamekuwa wakisaidia serikali hiyo yenye makao yake Mogadishu.
Januari mwaka
uliopita, wapiganaji wa al-Shabab walishambulia kambi ya majeshi ya Kenya
el-Adde na kuua wanajeshi wengi.
Al-Shabab
walisema waliua zaidi ya wanajeshi 100. Jeshi la Kenya halijatangaza idadi
kamili ya wanajeshi waliouawa hadi wa leo.
CHANZO: BBC
SWAHILI
No comments:
Post a Comment