Promosheni
ya ‘Nogesha Upendo’ iliyozinduliwa mwezi uliopita imemalizika leo ambapo
imewawezesha watumiaji wengi wa mtandao huo kujishindia fedha
taslimu na vifurushi vya muda wa maongezi na intanenti.
Meneja
Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu,amesema kuwa promosheni hiyo imekuwa na
mafanikio makubwa na kufanikisha lengo lililokusudiwa na kuwapa watumiaji wa
mtandao huo zawadi ya kipekee.
“Hadi
kufikia sasa wateja wapatao 400 wameweza kujishindia fedha taslimu
shilingi milioni 1/-kila mmoja na wateja zaidi ya 1,200 wamejishindia fedha
taslimu shilingi laki 1/-kila mmoja na wapo maelfu ya wateja ambao wamezawadiwa
dakika za muda wa maongezi na MB za intanenti bure”.Alisema Nkurlu.
Alisema
Vodacom inayo furaha kuona promosheni hii imewezesha maisha ya wateja wake kuwa
murua na itaendelea kubuni promosheni nyingine zenye lengo la kubadiilisha
maisha ya wateja nahuduma mbalimbali za kuwapeleka watanzania katika ulimwengu
wa kidigitali.
”Tunawashukuru
sana wateja wetu wote walioshiriki katika promosheni hii kwa kuendelea kuwa
katika familia ya Vodacom na tunawaahidi kuendelea kuwapatia huduma bora wakati
wowote na mahali popote.
No comments:
Post a Comment