Saturday, May 21, 2016

Man UTD watwaa ubingwa wa FA wakiwa 10 uwanjani.

Kitwanga
Manchester United wametoka nyuma na kuichapa Crystal Palace na kutwaa kombe la FA Cup kwenye uwanja wa Wembley kupitia goli la ushindi la Jesse Lingard katika muda wa nyongeza baada ya sare ya goli 1-1 kwenye dakika 90.
Huku kukiwa na tetesi kwamba mchezo huo huenda ukawa wa mwisho kwa kocha Louis van Gaal kama manager wa Manchester United, lakini ameweza kuongeza taji maarufu kwenye maisha yake ya soka akiwa England.
Kitwanga 5
United wangelikosa taji hilo inamaanisha walikuwa wanamaliza msimu huu bila taji lolote huku wakiwa wameshapoteza nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya, Jason Puncheon aliongeza maumivu kwa United baada ya kukandamiza bao lililoiweka mbele Palace zikiwa zimesalia dakika 12 pambano kumalizika.
Kitwanga 4
Goli la Puncheon lilikuwa ni mwiba kwa United lakini wakali hao wa Old Trafford walisawazisha bao hilo dakika nne baadaye kwa Mata kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Wayne Rooney.
Kitwanga 6
Beki wa Manchester United Chris Smalling alioneshwa kadi ya pili ya njano na kusindikizwa na kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Yannick Bolasie wakati wa muda wa nyongeza lakini Lingard akapeleka shangwe Old Trafford kwa kufunga bao la ushindi na kuipa United taji la FA.
Je, wajua?
  • Manchester United sasa wametwaa FA Cup kwa mara ya 12 na kuifikia rekodi ya Arsenal
  • Louis van Gaal ni kocha wa tatu kutoka Uholanzi kufanikiwa kushinda FA Cup, akitanguliwa na Guus Hiddink na Ruud Gullit.
Kitwanga 1
  • Goli la ushindi la Jesse Lingard lilikuwa la kwanza kwenye michezo 18 aliyocheza kwenye mashindano yote.
Kitwanga 2
  • Chris Smalling ni mchezaji wanne lakini ni wa kwanza kutoka England kupewa kadi nyekundu kwenye mchezo wa fainali ya FA Cup wengine waliowahi kupewa kadi nyekundu kwenye fainali ya FA Cup ni (Kevin Moran 1985, Jose Reyes 2005 and Pablo Zabaleta 2013).
Kitwanga 3
  • Manchester United wameshinda michezo yote ya fainali za FA Cup iliyohusisha wachezaji wake kutolewa kwa kadi nyekundu (1985 and 2016).  
CHNANZO: shaffhdauda.co.tz

No comments: