Mbunge wa Newala mjini (CCM) Mhe. George Mkuchika, akichangia jambo katika kikao cha bodi ya barabara. |
Mbunge wa viti maalum (Chadema), Tunza Malapo, akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kikao cha bodi ya barabara wiki mbili zilizopita mjini Mtwara. |
Na Juma Mohamed, Mtwara.
MBUNGE wa Newala mjini (CCM), Mhe. George
Mkuchika, amepingana na sehemu ya taarifa iliowasilishwa na sekta ya kilimo
katika kikao cha Baraza la Ushauri la Mkoa (RCC) inayoeleza kuwa sherehe za
unyago hazina ulazima hivyo zinachangia matumizi mabaya ya chakula.
Akizungumza
mbele ya mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti
wa kikao hicho, Mkuchika alidai kuwa kipengele hicho kilimchefua kwasababu kila
kabila katika nchi hii lina mila na desturi zake, hivyo sio vizuri kukosoa mila
za kabila Fulani pasipo kujua faida zake.
“Nataka
niwaambie, wiki mbili zilizopita kulikuwa na hotuba ya baba wa Taifa na alikuwa
anasema juu ya waandishi wa habari, akasema wasomaji tunapenda kusoma habari
zilizoandikwa vizuri na zenye elimu nzuri, na mwalimu akasema ipo elimu
nyingine hauipati kwenye magazeti na akasema kwa mfano elimu ya jandoni..kwahiyo
Baba wa Taifa wan chi hii anajua kuwa Jandoni kuna elimu..” alisema na
kuongeza:
“Leo
mumekuja kuleta ‘paper’ hii mlijua hapa kuna Wamakua, Wayao, Wamakonde, Wamwela
ambao wana mila na desturi za unyago..naombeni sana mtukome na muache..”
aliongeza.
Mbunge wa Tandahimba (CUF), Katan Ahmed, akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kikao cha bodi ya barabara wiki mbili zilizopita mjini Mtwara. |
Alitumia
muda mrefu kuwaeleza wajumbe wa kikao hicho mambo mbalimbali yanayohusu jando
na unyago ambapo alisema katika makabila ya Mtwara na Lindi wanapitia katika
hatua zaidi ya Tano kwa watoto wanaokuwa kwenye Jando ikiwa pamoja na kupelekwa
Jandoni, Kualuka na Kuolewa ambapo kunaambata na kikao cha kumfunda yeye na
mume wake vie watakavyoishi katika ndoa yao.
Alisema kuwa
majukumu hayo yanatekelezwa na watu wazima na kudai kuwa hata kwa wajumbe ambao
walikuwepo kwenye kikao hicho hakukuwepo ambaye ana umri unaofanana nao, na
kwamba hata yeye alikaa porini kwa ajili ya unyago kwa kipindi cha miezi
Miwili.
“Anatoka
Jandoni motto anaambiwa ni marufuku kwenda chumbani kwa baba na mama..ndio
maana mdogo wako ukigombana naye ambaye hajaaluka anakuchokoza alafu
anakimbilia chumbani kwa baba na mama ni kwasababu anajua wewe uliyealuka
huwezi kuingia kule, sasa jamani mambo haya ni kuheshimiana, mimi nina uhakika
Wanyamwezi wana taratibu zao kuelimisha watoto wao na Wasukuma na wengine.”
Alisema.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akizungumza katika kikao cha bodi ya barabara. |
“Nafikiri ni
mwandishi tu aliteleza kuliweka vizuri, kuna shughuli zingine tunazifanya kwa
kusherehesha ambazo zinasababisha kaya kuingia kwenye njaa pasipo sababu za
msingi lakini sidhani kama yupo mtu mzima hapa atadharau maana ya jando na
unyago, na watoto wetu wanakosa kwa kiwango kikubwa ndio maana wanapungukiwa
kwenye mengi lakini kwa wengine ambao tumepita huko tunaelewa maana yake
Mheshimiwa..kwahiyo tuko pamoja, kweeeeeli tumekoma” alisema.
No comments:
Post a Comment