Na Juma Mohamed, Mtwara.
WAFANYABIASHARA
Wanne raia wa Tanzania wameuawa nchini Msumbiji watatu kati yao wakipigwa
risasi baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliokuwa na
silaha za moto na mapanga.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe,
alisema wafanyabiashara hao wa Dhahabu walivamiwa wakiwa katika vibanda vyao
vya kubadilishia fedha usiku wa Februari Nane mwaka huu na kiasha kushambuliwa
kwa risasi na mapanga ambapo baadhi yao walifariki papo hapo na wengine
walifariki baada ya kufikisha hospitalini.
Alisema
waliouwawa katika tukio hilo ni Salumu Mfanga (44) mkazi wa Temeke, Dar es
Salaam, Yusuph Twalibu (34) mkazi wa Tanga, Hamisi Mkapila (40) mkazi wa
Morogoro na Mariam Ramadhani mkazi wa Tanga ambaye yeye hakupigwa risasi
isipokua alifariki kwa kukosa huduma baada ya kuvunjika mguu wakati anakimbia
kujiokoa.
Henry Mwaibambe |
“Kwahiyo
ndugu zao ambao wanaishi kule Msumbiji ndio ambao walikuja hapa (Mtwara) na
maiti, sasa utaratibu tuliofanya kwasababu tukio limetokea katika nchi jirani
ya Msumbiji ni kwamba sisi hawa marehemu tuliwapeleka Mochoale ya hospitali ya
mkoa ya Rufaa ya Ligula kwa ajili ya uchunguzi kwasababu tulipata taarifa
kwamba waliuwawa na tumethibisha kwamba kweli wameuwawa na wana majeraha ya
lisasi na wengine majeraha ya vitu vyenye ncha kali kama vile panga au visu..”
alisema.
Alisema
kutokana na marehemu hao kuwa sio wakazi wa Mtwara, ilitolewa ruhusa ya
kuisafirisha miili yao na baadhi ya ndugu na jamaa ambao waliipokea miili hiyo
kwa ajili ya kuisafirisha mpaka sehemu husika kwa ajili ya shughuli nyingine za
mazishi.
“Msumbiji ni
majirani zetu, na kwamujibu wa ndugu wa marehemu ni kwamba tukio lilitokea
katika kijiji cha Mtoro, wilaya ya Mtepweshi kwahiyo tutafanya mawasiliano na
wenzetu wa Msumbiji tujue namna gani tukio hili lilivyo..kwa taarifa ya ndugu
wa marehemu ni kwamba jalada kule limeshafunguliwa, lakini na sisi kwa taratibu
zetu tutawasiliana na ngazi ya mkoa ili tuweze kujua namna gani wenzetu hawa
wafanyabiashara tukio hili limewakuta na kuweza kuuwawa..” alisema.
Kwa upande
wa ndugu wa marehemu, Doto Ramadhani Mfanga, alisema marehemu hao walipigwa
risasi na wawili kati yao walifariki papo hapo huku wawili wengine walifariki
njiani wakati wakipelekwa hospitalini ambao ni Salumu Mfanga na Mariam
Ramadhani.
Alisema watu
hao baada ya kutekeleza mauwaji hayo walifanikiwa kuchukua fedha ambazo thamani
yake ni sh. Milioni 20 zilizokuwa za marehemu mmoja ambaye ni Salum Ramadhani,
pamoja na dhahabu ambazo hazikufahamika ni za thamani gani.
“Mimi tukio
wakati linatokea nilikuwa Nampula, nikapata taarifa siku ya Jumatatu saa Sita
mchana kwamba tuko hapa njiani tunampeleka mjomba wako hospitalini lakini
amefariki wakati tunampeleka hospitalini ndio wakanielezea mkasa mzima
ulivyotokea.” Alisema.
Kaimu mganga
mkuu wa hospitali ya rufaa ya Ligula mkoani hapa, Dickson Sahini, alipotafutwa
kwa ajili ya kuelezea tukio hilo alidai kuwa hana taarifa hizo na kushindwa
kutolea maelezo.
No comments:
Post a Comment