Friday, February 5, 2016

TPDC kuanza mradi mpya wa kusambaza gesi Mtwara na Lindi.

Meneja wa biashara ya gesi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Emmanuel Gilbert, akiwasilisha mada katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa Mtwara juu ya uelewa katika sekta ya Mafuta na Gesi iliyoandaliwa na shirika hilo.



Viongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wa mkoa wa Mtwara, baada ya kumalizika kwa semina ya siku moja ya kuwajengea uwezo waandishi juu ya uelewa wa sekta ya Mafuta na Gesi, iliyoandaliwa na shirika hilo



Waandishi wa habari wa mkoa wa Mtwara wakiwa katika semina ya siku moja ya kujengewa uwezo wa uelewa wa sekta ya Mafuta na Gesi iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania


Meneja wa kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba, mkoani Mtwara, Leons Mroso, akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari wa mkoa Mtwara katika semina ya siku moja ya kuwajengea uwezo wa uelewa katika sekta ya Mafuta na Gesi


Na Juma Mohamed, Mtwara.

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema lipo kwenye mchakato wa ujenzi wa mradi wa usambazaji wa gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya majumbani, viwandani na kwenye magari katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Hayo yamezungumzwa juzi mkoani hapa na meneja wa biashara ya gesi wa shirika hilo, Emmanuel Gilbert, baada ya kumalizika kwa semina ya siku moja ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa Mtwara juu ya uelewa wa sekta ya Mafuta na Gesi iliyoandaliwa na shirika hilo.
Alisema tayari upembuzi yakinifu umeshafanyika katika maeneo yatakayopitiwa na mradi huo na kwamba sasa shirika hilo linasubiri kupatiwa fedha kutoka serikalini kwa ajili ya kufanya usanifu wa michoro katika maeneo hayo yatakayojengwa miundombinu hiyo.

Meneja wa biashara ya gesi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Emmanuel Gilbert, akiwasilisha mada katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa Mtwara juu ya uelewa katika sekta ya Mafuta na Gesi iliyoandaliwa na shirika hilo.


Alisema, licha ya kusubiri pesa hizo jitihada zinazofanywa na shirika kwa sasa ni kujaribu kuzihusisha sekta binafsi kwa ajili ya kuleta mitaji ambayo itasaidia kupatikana pesa za kuanza shughuli hiyo.
“Serikali kama serikali vipaumbele ni vingi, ukisema tu kwamba wanapeleka pesa nyingi kwenye hii miundombinu kwa ajili ya uwekezaji kwenye hii miundombinu ambayo inahitaji pesa nyingi kwa ajili ya kuendelezwa..kwahiyo sisi kama TPDC tumekuwa tukijitahidi sana kuhakikisha kwamba tunawaleta watu wa sekta binafsi ili waweze kuleta mitaji kwa ajili ya kuendeleza hiyo miundombinu..” alisema.
Alisema, mradi huo ambao kuanza kwake kunategemea na upatikanaji wa fedha, mtandao wake wa kutandaza mabomba utakuwa na urefu wa Km 17 kwa mkoa wa Mtwara ambapo unatarajiwa kuunganisha nyumba 11,000 na magari 4,000 ambayo yatakuwa na yanauwezo wa kuamua kutumia nishati ya gesi au mafuta, na Km 11 kwa mkoa wa Lindi.
“Hiyo siyo ‘limit’ kwamba ndiyo mwisho, hiyo project ya kwanza itakapo kamilika na kama pesa zitaendelea kupatikana mradi utakuwa unapanuka..na niwaambie tu wananchi wa Mtwara kwamba tunahitaji ‘support’ yao, na yale yaliyotokea nyuma ni kwamba tu kwasababu ya kukosekana kwa taarifa kwamba upande mmoja ulikuwa na taarifa na mwingine haukuwa na taarifa na sasa hivi tumejitahidi sana kuhakikisha tuna ‘close’ hiyo ‘gape’..” aliongeza.
Kwa upande wake, meneja wa utafiti wa shiika hilo, Venosa Ngowi, alisema shirika kwa sasa lipo katika hatua za kushughulikia ujenzi wa miundombinu katika mtambo wa kupokea na kuchakata gesi kuibadilisha kutoka kwenye hewa na kuwa katika kimiminika, ambapo kwa kitaalamu huitwa Liquefied Natural Gas (LNG).

Afisa mahusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania-Maria Mselemu, akizungumza jambo katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mkoa wa Mtwara juu ya uelewa wa sekta ya Mafuta na Gesi.


Alisema, mtambo huo ambao utajengwa katika eneo la Likongo mkoani Lindi na kukamilika kwake kunatarajiwa kuwa baada ya miaka Minane hadi kumi ambapo utagharimu kiasi cha dola za kimarekani Billion 30-60.
“Gesi hii tunaisimika kwenye nyuzi -162 C alafu tunaisafirisha kuipeleka kwenye masoko na mradi huu ni mkubwa tunafanya pamoja na makampuni ambayo yamegundua gesi baharini, tunafanya pamoja na Statoil ya Norway, BG pamoja na Ophir Energy.” Alisema.

Katibu wa Chama cha Waaandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara, Bryson Mshana, akichangia jambo katika semina ya kuwajengea uwezo waandshi wa habari wa mkoa wa Mtwara juu ya uelewa wa sekta ya Mafuta na Gesi, iliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania





No comments: