Monday, February 1, 2016

Simba wazindua Duka la kuuza bidhaa zao..

Rais wa klabu ya Simba (katikati) akikata utepe kuzindua duka la kuuza vifaa vya Simba lililopo DarFree Market Mall Ground Floor
Rais wa klabu ya Simba (katikati) akikata utepe kuzindua duka la kuuza vifaa vya Simba lililopo DarFree Market Mall Ground Floor

Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva (katikati) akikata utepe kuzindua duka la kuuza vifaa vya Simba lililopo Dar Free Market Mall Ground Floo

Klabu ya Simba SC leo imeamua kufanya kweli baada ya kuzungumza mambo mengi ambayo mwisho wa siku yalikuwa yamebaki kwenye makaratasi. Simba leo wamezundua rasmi duka ambalo litakuwa linauza vitu mbalimabali vyenye nembo ya klabu hiyo kwa lengo la kutengeneza mkwanja.
DSC_0350
DSC_0350
Imekuwa muda mrefu sasa tangu vilabu hivyo viwili vya Simba na Yanga vilipoanza kupiga kelele za kuhakikisha bidhaa zenye nembo za klabu zao zinavinufaisha vilabu lakini bado wajanja waliendelea kufaidika kutokana na vilabu hivyo kushindwa kudhibiti watu ambao wamekuwa wakipiga pesa kwa kuuza bidhaa zenye nembo za vilabu hivyo.
IMG_2260
IMG_2260
Rais wa Simba Bw. Evans Aveva leo amezindua rasmi duka la Simba ambalo litakuwa likiuza vifaa vya michezo, jezi, kofia, T-shirts pamoja na vitu vingine vingi vyenye chapa ya Simba kwa ajili ya kujiingizia kipato kutokana na chapa ya timu yao.
DSC_0352
DSC_0352
Hiyo ni changamoto kwa vilabu vingine vya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ambavyo bado vimelala huku wajanja wa mjini wakiendelea kuponda pesa kutokana na kuuza bidhaa zenye nembo zao huku wao wakiwa hawapati hata shilingi 100.
SOURCE: shaffihdauda.co.tz
DSC_0349


No comments: