Thursday, February 11, 2016

Mourinho azidi kupigiwa upatu Man Utd..

Mourinho
Jose Mourinho ndiye afaaye zaidi kusaidia Manchester United kukabiliana vilivyo na Manchester City watakaokuwa chini ya Pep Guardiola msimu ujao, haya kwa mujibu wa mshambuliaji wa zamani wa Porto Benni McCarthy.
BBC imefahamu kwamba huenda Mourinho, 53, aliyekuwa meneja wa Chelsea, huenda akateuliwa kumrithi Louis van Gaal kama meneja Old Trafford majira yajayo ya joto.
McCarthy, 38, alicheza chini ya Mourinho raia huyo wa Ureno alipokuwa mkufunzi wa Porto.
"Mourinho ni mmoja wa watu wanaojua jinsi ya kumshinda Guardiola na mbinu zake,” ameambia BBC Sport.
Porto
“Alipokuwa Real Madrid, alimshinda mara kadha. AKiwa Inter Milan, alifanikiwa pia dhidi yake (Guardiola).
"Kwa sasa sioni mtu yeyote anayeweza kumkabili Pep na mbinu zake Manchester City isipokuwa tu Mourinho akiwa United, atakwua na rasilimali, wachezaji na usaidizi wa kifedha wa kukabiliana na Guardiola."
Guardiola, alikuwa kocha wa Barcelona, kwa sasa ni mkufunzi mkuu wa Bayern Munich.
Klabu ya Manchester City ilitangaza majuzi kwamba atamrithi Manuel Pellegrini majira yajayo ya joto.
Mourinho alifutwa kwa mara ya pili Chelsea mwezi Desemba, baada ya kushindwa mechi tisa kati ya 16 za kwanza ligini.
Alifutwa kazi miezi saba tu baada ya kuongoza klabu hiyo kushinda Ligi ya Premia.
Alikuwa Chelsea kwa kipindi cha kwanza 2004-2007.
SOURCE: BBC SWAHILI

No comments: