Wednesday, September 23, 2015

Wanachama PPF watakiwa kuchangamkia 'Wote Schem'

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mohamed Gharib Bilali, akizungumza na Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF kanda ya kusini, Kwame Temu, alipokuwa akikaguwa mabanda ya maonyesho katika kilele cha maadhimisho ya siku ya bahari Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mtwara jana.





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mohamed Gharib Bilali, akizungumza na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Makontena Tanzania (TICTS), Donald Talawa, alipokuwa akikaguwa mabanda ya maonyesho katika kilele cha maadhimisho ya siku ya bahari Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mtwara jana.




Wadau wa huduma za majini na viongozi mbalimbali waliojitokeza katika viwanja vya Bandari mkoani Mtwara, katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, yaliyofanyika jana na kuhitimishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mohamed Gharib Bilali.

 Na Juma Mohamed, Mtwara.

WANACHAMA wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF walio katika sekta rasmi na zisizo rasmi wametakiwa kujiunga katika fao jipya la Wote Sceme, linalomuwezesha mwanachama kupata mafao ya afya kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).


Akizungumza na NEWS ROOM mkoani Mtwara, meneja wa mfuko huo kanda ya kusini, Kwame Temu,  alisema faida nyingine ambazo mwanachama atazipata ni pamoja na mikopo mbalimbali inayotolewa na benki ya posta, kupata mafao ya uzeeni pamoja na kunufaika na fao la uzazi kwa akina mama ambao watakuwa wamejifungua.


Aidha, amesema kutokana na fao hilo kuwa jipya ambapo lilizinduliwa mwezi Julai mwaka huu, wanatoa elimu kwa wanachama kupitia semina mbalimbali kwa waajiri, vyombo vya habari na vipeperushi mbalimbali ambavyo wamevigawa katika maeneo mengi ya nchi.


“Tunawafikia wanachama wetu kupitia semina mbalimbali amabazo tunazitoa kwa waajiri, lakini pia vilevile kupitia VICOBA, SACOS, kwenye vyombo vya habari kama hivi..pia vipeperushi mbalimbali ambavyo tumevigawa katika maeneo mengi ya nchi..lakini kwa kiasi ni kupitia tunawaelimisha kupitia semina..” alisema.

No comments: