|
Ibrahimu Issihaka wa Ndanda Sc akiruka kuwania mpira na mchezaji wa Mgambo JKT
|
|
Wachezaji wa Ndanda Sc na Mgambo JKT wakiingia uwanjani kwa ajili ya kuanza mchezo
|
|
Wachezaji wa Ndanda Sc na Mgambo JKT baada ya kukaguliwa na kamisaa wa mchezo
|
|
Wachezaji wa Ndanda Sc na Mgambo JKT wakipeana mikono pamoja na waamuzi.
|
|
Kikosi cha Ndanda Sc ya Mtwara, kilichoanza katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mgambo JKT ya Tamga.
|
|
Kikosi cha Mgambo JKT ya Tanga, kilichoanza katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda Sc ya Mtwara
|
|
Benchi la Mgambo JKT
|
|
Benchi la Ndanda Sc
|
Timu ya soka
ya Ndanda Sc ya mkoani Mtwara imeshindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani
wa Nangwanda Sijaona, baada ya kulazimishwa sare ya goli 1-1 na Mgambo JKT ya
Tanga, katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara.
Ndanda ndio
walioanza kupata goli kupitia kwa mshambuliaji wao mpya Atupele Green,
aliefunga goli la mapema dakika ya pili ya mchezo baada ya kuwazidi ujanja
walinzi wa Mgambo, kabla ya Fullu Maganga kusawazisha katika dakika ya 72
kutokana na makosa binafsi yaliyofanywa na walinzi wa Ndanda.
|
Kashikashi langoni mwa timu ya Mgambo JKT
|
Akizungumza baada
ya mchezo huo, kocha wa Ndanda Sc, Amimu Mawazo, amekiri kuwepo kwa makosa yaliyofanywa
na wachezaji wake kiasi cha kuwakosesha kuondoka na pointi tatu katika mchezo
huo.
“Kwasababu
nimeshagundua makosa ni nini sasa naogopa sana kwenye vyombo vya habari, maana
yake nikirudi tena nakuwa na walewale ambao wamefanya makosa, kwahiyo
nimelichukuwa mimi kama mwalimu nakwenda kulifanyia kazi..” alisema.
Na kuongeza “wapinzani
wangu wamecheza vizuri na wamecheza kimpira na wameshinda kimpira, kwenye kosa
ambalo tumelifanya sisi wao wamepata ‘advantage’ na wameza kupata goli kwahiyo
huo ndio mpira.” Aliongeza.
Kwa upande
wake, kocha wa Mgambo JKT, Bakari Shime, amesema lengo lao limetimia kwasababu
waliingia katika mchezo huo kwa tahadhari kubwa huku wakitafuta matokeo ya sare
kutokana na kuwahofia wapinzani wao.
|
Nahodha wa Ndanda Sc, Kiggi Makasy, akichuana na Nahodha wa Mgambo JKT, Fullu Maganga.
|
“Tuliingia
kwa kutafuta alama moja, lazima niseme ukweli, lakini kama mulivyoona
tulifungwa goli la mapema sana ambalo lilituchanganya, lakini tulirudi mchezoni
baadaye na tukafanya ‘substitute’ (Mabadiliko) tukamuingiza mchezaji wetu
wakutegemewa lakini akaumia mkono mda uleue..kwahiyo kimsingi hali yetu ilikuwa
ngumu kidogo lakini nawashukuru vijana wangu walirudi mchezoni na mwisho wa
mechi tukapata alama moja.” Alisema.
Kwa upande
wa mashabiki, wanasema bado timu yao haijakaa sawa kiasi cha kuwaridhisha,
lakini wanaimani na benchi la ufundi litafanya kazi yake ipasavyo na kwamba
mechi zijazo watafurahi.
No comments:
Post a Comment