Mizengo Pinda, kulia. |
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akikagua banda la Poly Mashine zinazotumika katika shughuli za kilimo. |
Noti mbalimbali za fedha za kitanzania zikiwa zimeharibiwa na Benki Kuu ya Tanzania, baada ya kujiridhisha kuwa zimechakaa. |
Waziri mkuu Mizengo Pinda, akiwa katika banda la Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mahusiano, Gaudensia Simwanza, kuhusu mambo yanayofanywa na mamlaka hiyo. |
Na Juma Mohamed, Lindi.
Wazri Mkuu
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda amesema Tanzania ni
miongoni mwa nchi kadhaa barani Afrika ambazo zina kiasi kikubwa cha chakula na
kupelekea kusaidia mataifa mengine.
Akizungumza jana
katika ufunguzi wa maonyesho ya kilimo (NANENANE) yaliyofanyika kitaifa katika
viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, Pinda alisema hivi karibuni zilitolewa tani 1,300
kwa ajili ya kuisaidia nchi ya Sudani huku tani 500 zikitolewa kuisadia Malawi.
Aidha, waziri
mkuu amekubaliana na ombi lililotolewa na mwenyekiti wa Chama cha Wakulima
Tanzania (TASO) Englibert Moyo, kutaka kanda ya kusini kuongezewa tena miaka
miwili zaidi ya kuendelea kuandaa maonyesho hayo kitaifa.
No comments:
Post a Comment